General Terms & Conditions

1. JUMLA
+

1.1. SportPesa ni jina la biashara la SportPesa Limited (hapa chini kurejewa kama "Kampuni"), ambayo ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania na yenye ofisi zake eneo la: Peninsula House, Plot 251, Toure Drive, S.L. P 23135 Dar es Salaam, Tanzania.

1.2. Kampuni hii inaendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria na inasimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Imepatiwa leseni namba SBI000000027 iliyotolewa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania chini ya Sheria ya Michezo ya Kubahatisha (Sheria Na. 4 ya mwaka 2003).

1.3 Makubaliano haya yanaweka Vigezo na Masharti (hapa chini kurejewa kama “Kanuni”) vitakavyotawala mahusiano ya kimkataba kati yako kama Msajiliwa/Mchezaji shiriki wa Kampuni na Kampuni. Kanuni hizi zitatumika katika uchezaji wako kupitia njia zote za mawasiliano ikiwemo majukwaa ya ki-elektroniki kama simu za kiganjani, kompyuta pamoja na kompyuta mpakato. Unatakiwa kukubaliana na Kanuni hizi wakati unapojisajili na kufungua akaunti yako kwenye Kampuni na unajifungamanisha kikamilifu na Kanuni hizi kwa muda wote wa mahusiano yako na Kampuni. Kampuni ina haki ya kukataa usajili ama ushiriki wako ikiwa ina sababu za kuamini kwamba taarifa unazozitoa sio sahihi amd inatilia shaka usafi wa fedha ama mienendo yako ambapo usajili wako waweza ahirishwa kwa muda ama kusitishwa kabisa.

1.4. Kanuni hizi zimenyambulishwa kurahisisha uelewa wake pamoja na rejea. Ni muhimu kusoma na kuelewa Kanuni hizi kama mchezaji. Matumizi ya maneno “wewe”, “ÿako”, mchezaji”” ama “mteja” au “mtumiaji” yanamaanisha mtu yeyote anayeshiriki kufanya ubashiri au anayetumia huduma ya Kampuni kupitia majukwaa mbalimbali yaliyowekwa na Kampuni kwaajili hiyo au mtu yeyote aliyejisajili na Kampuni. Maneno “Kampuni”, “sisi”, “yetu” ama “sisi” yatamaanisha Sportpesa Limited, SportPesa pamoja na warithi ama wateule wake.

1.5. Kampuni ina haki ya kubadili Kanuni hizi muda wowote na bila notisi ya awali. Kampuni itafanya liwezekanalo kukujulisha juu ya mabadiliko yoyote makubwa ya Kanuni hizi. Hata hivyo, ni wajibu wako kuangalia mara kwa mara kama kuna mabadiliko yoyote. Iwapo kutokana na kuwepo kwa mabadiliko hayo hutopenda kuendelea kutumia huduma za Kampuni, waweza kutoa pesa zako ambazo hujacheza bila faini na kufunga akaunti yako kwa kutuma barua pepe kwenda: tz.customercare@sportpesa.com ukieleza nia ya kufanya hivyo. Kampuni itakujibu kuthibitisha kupokea maamuzi yako ya kutoendelea kutumia huduma zake. Hata hivyo, ikitokea hujajibiwa, haitamaanisha hata kidogo kuwa Kampuni ina wajibika kwa jambo lolote kufuatia kujitoa kwako.

1.6. Kampuni itaheshimu usiri na faragha yako kulingana na sera ya Kampuni juu ya faragha, na itajitahidi kadri ya uwezo wake kutunza, wakati wote, taarifa zako kwa usiri mkubwa. Hata hivyo, Kampuni haitowajibika kutokana na upotevu wa taarifa aidha zikiwa mikononi mwake yenyewe ama watoa huduma wake huru ambao Kampuni itawategemea aidha kwa ujumla au kwa sehemu kutoa huduma.

1.7. Kampuni haitatoa taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote isipokuwa kama:

  • 1.7.1. inahitajika ili kushughulikia maombi yako;
  • 1.7.2. ni wajibu na/au takwa la kisheria kwa Kampuni;
  • 1.7.3. inahitajika ili kutekeleza matakwa ya Kanuni hizi ama makubaliano mengine;
  • 1.7.4. inahitajika ili kulinda haki za Kampuni au mali, ikiwa ni pamoja na kubadilishana taarifa na makampuni na mashirika mengine kwa madhumuni ya kuthibitishaukweli wa taarifa hizo, ulinzi dhidi ya udanganyifu na kupunguza hatari itokanayo na mikopo. Taarifa binafsi unazotoa zaweza kutolewa kwa shirika la mikopo, ambalo laweza kutunza kumbukumbu ya taarifa hizo.

1.8. Mahusiano ya kimkataba baina yako na Kampuni yanaongozwa na Kanuni hizi pamoja na sheria husika za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo ndio Mamlaka Kampuni inaendeshea shughuli zake za kutoa huduma aidha moja kwa moja kwa wachezaji waliosajiliwa na/au kupitia kwa watoa huduma wake au mawakala wake.

1.9. Kwa kukubaliana na Kanuni hizi, na utakapocheza mchezo wowote, ama kufanya ubashiri wako kupitia njia zilizowekwa na Kampuni, unakubali kufungwa kikamilifu na masharti ya Kanuni hizi pamoja na marekebisho yake na pia kanuni za mchezo husika kama utakavyotolewa na Kampuni mara kwa mara. Unakiri kwamba Kampuni itakuwa na haki ya kutumia, mara kwa mara, taarifa zote zilizokusanywa kwaajili ya kufanya utafiti wa masoko, dodoso juu ya kiwango cha huduma kwa wateja, masoko na kutangaza huduma zake na zile za washirika wake.

1.10. Kiasi chochote ambacho mchezaji atashinda kitakatwa kodi ya asilimia kumi na tano (15%) ya kiasi hicho kulingana na matakwa ya Serikali ya Tanzania.

1.11. Kampuni haitowajibika kwa madhara yoyote yatokanayo na matukio makubwa kama vile mgomo wowote, vitendo vya kigaidi, mgogoro wa kisiasa, vita, janga la asili na kuchujika kwa mitandao ya maswasiliano, mashambulizi ya kimtandao, uvamizi wa mitambo n.k, ambayo inaweza kusababisha kwa ujumla au kwa kiasi upungufu katika kupatikana kwa huduma, kupotelewa kwa taarifa za Kampuni au za watoa huduma wengine wa kujitegemea ambao Kampuni itakuwa inawategemea ili kuipatia huduma.

2. KUFUNGUA AKAUNTI & KUJISAJILI
+

TARATIBU ZA AKAUNTI

2.1. Ili kuweza kubashiri au kucheza mchezo, utatakiwa kufungua akuanti. Ili uweze kufungua akaunti ni lazima uwe na umri unaokubalika kisheria na ufungue akaunti wewe mwenyewe. Lazima uandike umri wako katika vipengele vilivyopo na kuthibitisha taarifa hiyo katika vipengele vya usajili. Kwa kufanya hivyo, watumiaji huthibitisha kwamba wana umri unaokubalika kisheria yaani usiopungua miaka 18. Kampuni ina haki ya kuomba uthibitisho wa umri kutoka kwa mteja yeyote yule na ina mamlaka ya kusitisha akaunti husika kwa muda mpaka pale nyaraka za kuridhisha zitakapotolewa. Jina la mchezaji LAZIMA liwe sawa na jina lililotumika wakati wa kujisajili na Kampuni na ni lazima lifanane na jina lililosajiliwa katika namba ya simu ya kiganjani. Ikiwa si hivyo, akaunti husika itasitishwa. Endpo akaunti itasitishwa, mteja husika atalazimika kuwasiliana nasi. Kila ubashiri uliofanywa kabla ya akaunti kusitishwa halali ukiwa na uwezekano wa kushinda au kushindwa. Iwapo katika hatua yoyote ile ikagundulika akaunti inamilikiwa na mtu mwenye chini ya umri unaohitajika kisheria, akaunti hiyo itafungwa mara moja na haitofunguliwa daima, na fedha zote zitakazokuwa katika akaunti hiyo zitataifishwa. Katika kila mazingira yanayotia shaka ya namana hiyo, Kampuni itatoa taarifa kwa mamlaka husika na mchezaji anaweza akapatwa na madhara makubwa. Kwa kushiriki katika huduma zetu, unakubali kutoa taarifa zote tutakazohitaji kuhusiana na kujiridhisha juu ya taarifa zako sahihi. Tutakuwa na haki ya kusitisha kwa muda au kuweka masharti kwa akaunti yako kwa namna tutakavyoona inafaa mpaka hapo tutakapojiridhisha vilivyo juu ya uthabiti wa taarifa zako.

2.2. Kwa kufungua Akaunti nasi na kwa kutumia Huduma zetu, unathibitisha kuwa kwa wakati wote:

  • 2.2.1 una umri wa miaka 18 au zaidi;
  • 2.2.2. Una uwezo kisheria wa kuingia katika mkataba;
  • 2.2.3. Upo katika eneo ambalo ni halali kufungua akaunti nasi na kutumia Huduma zetu;
  • 2.2.4. Wewe ni mtu kama unavyotamka kuwa katika usajili wako, na unatoa taarifa sahihi, za wakati huu na kamilifu, na kwmba utarekebisha taarifa utoazo kwetu endapo zitabadilika;
  • 2.2.5. Unajisajili kama mhusika mkuu na si kwa niaba ya mtu mwingine;
  • 2.2.6. Hujawahi kuwa na akaunti ambayo imepata kufungiwa nasi au na mwendeshaji wa michezo ya kubahatisha kwa sababu za ukiukaji au matumizi mabaya au tabia iliyo kinyume cha sheria;
  • 2.2.7. Hujazuiliwa kwa sababu yoyote ile kubashiri au kutumia Huduma za Kampuni yetu; na
  • 2.2.8. Hujajiondoa au kukatazwa na mtu mwingine yeyote, ikiwemo Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, kujihusisha na michezo ya kubahatisha nchini. Utakapofungua akaunti yako, utapaswa kutupatia taarifa zako binafsi, ikiwa ni pamoja na Jina lako, tarehe ya kuzaliwa na anuani yako kamili pamoja na anuani ya barua pepe.
  • 2.2.9. Kwa kujisajili na Sportpesa, aidha kupitia mtandao wetu au kupitia nambari 15888, umekubali kupokea huduma ya taarifa za mchezo. Utapokea taarifa mara kwa mara kuhusu michezo mbalimbali na matangazo mengine. Ile kujitoa, wawezatuma neon “ONDOA” au “ACHA” kwenda nambari 15888

2.3 Unakubali kufuata Kanuni hizi wakati wote, na:

  • 2.3.1. Si kushiriki kwa faida/manufaa ya mtu wa tatu
  • 2.3.2. kutotumia fedha iliyopatikana kwa njia haramu
  • 2.3.3. kutokutoa pesa kwenye akaunti benki/kadi ya benki usiyo na mamlaka ya kutumia.
  • 2.3.4. kutokujaribu kuvamia mifumo ya Kampuni ya huduma za kifedha kwa njia ya simu, tovuti na njia zote zingine za habari / majukwaa ya kielektroniki au kubadili nywila kwa njia yoyote ile kwa nia ya kudanganya, au kulaghai mfumo au kwa njia yoyote kufanya udanganyifu au uhalifu wowote;
  • 2.3.5. kutojihusisha na vitendo vyovyote vya kihalifu dhidi ya Kampuni, washirika wake, wateja wake au mtu mwingine yeyote.
  • 2.3.6. kutoipotosha Kampuni kwa makusudi kwa kutoa taarifa za uwongo kama vile kutoa taarifa za uwongo wakati wa kufungua akaunti, kughushi nyaraka, kuficha utambulisho wako, tabia ya kutokuwa mkweli au kuficha mahala unapoishi na/au umri.

2.4. Iwapo ukikiuka kanuni moja au zaidi za Akaunti kama zilivyotajwa kwenye vifungu 2.1, 2.2 na 2.3, Kampuni ina haki ya kufunga akaunti yako na kushikilia fedha zozote zilizopo. Hali kama hiyo ikishukiwa, Kampuni itaripoti vitendo hivyo kwenye mamlaka husika na mchezaji anaweza kupata madharaa. Wajibu wa kimtakaba utaheshimiwa isipokuwa kama kuna ukiukwaji wa kipengele chochote cha kanuni hizi kwa upande wako au kukiuka sheria yoyote ya kimataifa na pia sheria za Tanzania. Michezo yakinifu itaongozwa kikamilifu na kanuni hizi pamoja na kanuni na miongozo mingine kama itakavyokuwa ikitolewa na Kampuni mara kwa mara. Michezo yote, miongozo na Kanuni vitabakia wakati wote kuwa mali ya Kampuni.

2.5. Ni wajibu wako kuhakikisha kuwa ha uvunji sheria yoyote katika mamlaka yako wakati wa kufungua akaunti na kufanya biashara na Kampuni muda wote ambao kujiunga / ushiriki wako unaendelea.Wakati wote usajili wako utakapokuwa hai, itakuwa ni wajibu wako kuhakikisha hukiuki sheria yoyote ya nchi wakati wa kufungua akaunti na kujishughulisha na Kampuni.

2.6. Lazima utoe taarifa sahihi wakati unapofanya usajili. Unakubali pia kufanyia marekebisho taarifa zako hizi pale zitakapobadilika.

2.7. Kampuni haitowajibika kwa vyovyote vile na kwa mtu yeyote kutokana nna wewe kutoa taarifa zisizo sahihi ama za uwongo.

2.8. Kila mteja atafungua akaunti moja tu. Tukigundua mteja yeyote ana akaunti zaidi ya moja, tuna haki ya kuzifunga akuanti zote.

2.9. Endapo Kampuni ikigundua kuwepo kwa akaunti nyingi zilizofunguliwa kwa makusudi kwa kutumia taarifa za uwongo, zikiwa na viashiria vya kijinai, ama iwapo Kampuni ikjiridhisha kuwa mmiliki wa akaunti ana nia ya kufanya udanganyifu, Kampuni itakuwa na haki ya kufunga akuanti hizo na kutaifisha fedha zote, ikiwa pamoja na amana ya awali. Hali kama hiyo ikishukiwa, Kampuni itatoa taarifa juu ya vitendo hivyo kwenye mamlaka husika na mchezaji anaweza kupata madhara. Ukimteua mtu mwingine kuwa na mamlaka ya kutumia akaunti yako, utawajibika kwa miamala yote ambayo mtu huyo ataifanya kwa kutumia taarifa sahihi za akaunti. Endapo utapoteza taarifa za akaunti yako au ukadhani kuwa mtu mwingine anaweza kuwa na taarifa zako za akaunti, tafadhali tujulishe mara moja. Hata hivyo, Kampuni haitowajibika kwa madhara yoyote utakayoyapata kutokana na miamala iliyofanywa na mtu huyo. Tafadhali tambua ya kuwa taarifa binafsi za usajili na taarifa zingine nyeti hazipaswi kutolewa kwa mtu au kutumwa kwetu kwa njia yoyote inayosomeka.

2.10. Kampuni hutunza akaunti za wateja na kuhesabu fedha zilizopo, fedha zinazosubiri kukamilika kwa muamala, fedha zilizokwisha kuchezwa pamoja na zawadi/ushindi. Mpaka hapo iktakapothibitishwa vinginevyo, vima hivi vya fedha huchukuliwa kuwa kamilifu na visivyo na mgogoro.

2.11. Miamala yote inafanyika kwa Shilingi za Tanzania. Hakuna riba inayolipwa kwenye pesa yoyote, bila kujali kiasi kilichopo kwenye akaunti yako au ucheleweshaji wowote katika kuweka pesa kwenye akaunti yako kwa sababu yoyote.

2.12. Kampuni sio taasisi ya fedha, na haitotumika kama wakala wa kutuma fedha, aidha zilizotumika ama zisizotumika, ikiwa ni kwa nia njema au kwa nia ovu. Aidha hutotumia Kampuni kama taasisi ya kubadilishia fedha. Endapo utafanya shughuli hizo kwenye akaunti yako, Kampuni ina mamlaka ya kufunga akaunti yako na/ au kuchukua fedha zozote zilizopo kwenye akaunti. Wajibu wa kimkataba utaheshimiwa daima, isipokuwa tu pale ambapo kipengele chochote cha Kanuni hizi kitakapovunjwa. Kampuni wala mfanyakazi wake hawatatoa mkopo, na bashiri zote bashiri zote lazima zifanyike kwa kutumia fedha za kutosha kutoka kwenye akaunti ya mteja. Kampuni ina haki ya kubatilisha ubashiri wowote ambao unawezakuwa umekubalika kimakosa wakati akaunti haina pesa za kutosha kulipia ubashiri. Endapo fedha zitawekwa kwenye akaunti ya mteja kimakosa, ni wajibu wa mteja kuifahamisha Kampuni mara moja. Kampuni itarejesha fedha hizo kwa kufanya marekebisho ya ki-akaunti.

2.13. Kampuni haitovumilia matusi, fujo au lugha/tabia chafu zitakazoelekezwa kwa wawakilishi wa Kampuni kupitia majukwaa yoyote ya huduma (maongezi, barua pepe, simu, sehemu za mauzo). Ikiwa utaamua kufanya mambo hayo, utapigwa marufuku kutumia njia yoyote kufikia huduma zetu na vitendo kama hivyo vitaripotiwa kwenye vyombo husika kwaajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

2.14. Utapaswa kutunza utambulisho wako pamoja na neno-siri (nywila) kwa siri kubwa wakati wote. Ni wajibu wako pekee kuhakikisha kuwa taarifa zako za siri zinakuwa salama. Endapo utahisi kuwa taarifa zako haziko salama, utapaswa kuwasiliana na Kampuni mara moja na kubadilisha taarifa zako za usalama mara moja. Kikiwa kwa wakati wowote akaunti yako itatumiwa na mtu mwingine bila ridhaa yako, Kampuni haitowajibika kwa jambo lolote litakalo jitokeza.

2.15. Jina-tumizi lako ni lazima iwe namba yako ya simu (ya kiganjani) iliyosajiliwa.

2.16. Ni marufuku kuuza na/au kuhamisha na/au kupata akaunti kwa/kutoka kwa wachezaji wengine. Hatua hiyo itasababisha kufungwa kwa akaunti na kutaifisha fedha zilizomo katika akaunti hiyo. Kampuni inaweza kwa hiari yake kurejesha akaunti hiyo ikiwa kuna ushahidi wa kutosha kuonesha kuwa uhamisho huo ulifanyika kimakosa.

2.17. Akaunti mfu ni akaunti ambayo haijapata kutumika kwa kipindi  cha miezi 6. Kutokutumika maana yake hakuna bet yoyote iliyofanywa au pesa iliyowekwa kwa wakati wowote ule au kutembelea akaunti katika kipindi hicho cha miezi sita. Akaunti ikishakuwa mfu, itatozwa kiasi cha shilingi 1000 (TZS 1,000.00) kwa mwezi kama tozo ya kutunza Akaunti  kuanzia Mwezi unaofuata baada ya Akaunti kuwa mfu. Mara miezi sita inakapoisha baada ya Akaunti kuwa mfu, Akaunti yoyote itakayokuwa haina salio la kutunza Akaunti itazuiwa na kufungwa mara moja. Mteja ambaye Akaunti yake itafungwa na anataka kuendelea kutumia huduma zetu atatakiwa kujisajili upya. Kwa madhumuni ya kuhesabu muda wa Akaunti kuwa mfu, kanuni zifuatazo zitazingatiwa:

2.17.2.1 Kwa mteja aliyejisajili lakini hajaweka pesa wala kutembelea akaunti, muda wa Akaunti yake kuwa mfu utaanza kuhesabiwa toka tarehe ya kujisajili au kutembelea akaunti

2.17.2.2 Kwa mteja aliyeweka pesa lakini hajacheza bet yoyote au kutembelea akaunti muda wa akaunti kuwa mfu utaanza kuhesabiwa kuanzia tarehe aliyoweka pesa mara ya mwisho au kutembelea akaunti

2.17.2.3 Kwa mteja ambaye amekuwa akicheza, muda wa Akaunti yake kuwa mfu utaanza kuhesabia kuanzia tarehe aliyocheza mara ya mwisho au kutembelea akaunti

2.18. Kampuni ina haki ya kusitisha mahusiano baina yake na mchezaji yeyot wakati wowote na kwa hiari ya Kampuni pekee. Kampuni pia ina haki ya kufunga au kusitisha kwa muda akaunti yako wakati wowote na kwa sababu yoyote. Bila kuathiri yaliyotangulia, Kampuni itakuwa na haki ya kufunga au kusitisha kwa muda akaunti yako endapo:

  • 2.18.1. ukifilisika;
  • 2.18.2. Kampuni itaona kuwa umetumia huduma/bidhaa/majukwaa yake kwa njia ya ulaghai au madhumuni yasiyo halali na/au yaliyo kinyume cha sheria au yasiyofaa.
  • 2.18.3. Kampuni inaona kuwa umetumia huduma / bidhaa / majukwaa kwa namna isiyo haki au umedanganya kwa makusudi au kufaidika na Kampuni ama wateja wake isivyo halali;
  • 2.18.4. Kampuni ikiombwa kufanya hivyo na polisi, mamlaka ya udhibiti yoyote au mahakama; au
  • 2.18.5 Kampuni inaona kuwa lolote kati ya yaliyotajwa katika vipengele (a) hadi (c) hapo juu limetokea au linaelekea kutokea.

2.19. Iwapo Kampuni itafunga au kusitisha kwa muda akaunti yako kwa sababu yoyote kati ya zilizotajwa hapo juu, utawajibika kwa madai yoyote, hasara, madeni, madhara au gharama zilizoingiwa ama kuikumba Kampuni (kwa pamoja 'Madai') kutokana na hayo na utairudishia na kutoihusisha Kampuni na madai hayo. Pia Kampuni itakuwa na haki ya kuzuia na/au kushikilia kiasi chochote cha fedha ambacho vinginevyo kingelipwa ama kingepaswa kulipwa kwako (ikiwemo fedha uliyoshinda au malipo ya ziada(bonasi).

2.20. Zaidi ya hayo, Kampuni itakuwa na haki ya kuzuia na/au kushikilia kiasi chochote na fedha yote ambayo utakuwa umepata au kupokea kutokana na au kuhusiana na kutumia huduma/bidhaa/majukwaa kinyume cha sheria ikiwa ni pamoja na kufanya vitendo vyenye malengo yasiyokusudiwa kisheria.

2.21. Ikiwa itathibitika kuwa Kanuni hizi ama sheria yoyote haijavunjwa, fedha yote inayopaswa kuwa kwenye akaunti itarudishwa kwa mchezaji kama uhusiano utakuwa umesitishwa na Kampuni. Kwa wakati wote, fedha yoyote ya mteja/mchezaji haitozwi riba, kwa mukhtadha huo, pesa yoyote inayorudishwa haitotozwi/katwa riba pia.

2.22. Kampuni inakataza na kuchukua hatua kali kupiga marufuku matumizi ya vifaa kama roboti, kompyuta zinazochujua uchezaji wa kawaida na halali. Endapo matumizi ya vifaa vya aina hii yakigundulika, Kampuni itampiga marufuku mchezaji/wachezaji husika, kufunga akaunti zao zote na kutaifisha fedha zote na mapato yote katika akaunti hizo. Hali hiyo ikishukiwa, Kampuni itatoa taarifa kwenye mamlaka husika na mchezaji anaweza kupata madhara.

3. KUWEKA, KUHAMISHA NA KUTOA PESA
+

3.1. Kwa amana zote, namba ya muwekaji lazima ifanane kabisa na namba ya simu iliyosajiliwa kwenye Kampuni wakati wa ufunguzi wa akaunti inayopokea fedha, yaani, akaunti iliyosajiliwa. Kama si hivyo, amana husika itakataliwa. Gharama zozote zitakazotozwa na makampuni ya sim kupitia huduma ya fedha kwa njia ya simu (Mpesa, Tigo pesa, Halopesa, Airtel Money na EzyPesa) zitakatwa kutoka kweye akaunti ya mchezaji. Una paswa kuweka pesa kwenye akaunti yako kwa madhumuni ya kucheza/kubashiri/ kupitia majukwaa ya Kampuni. Tutakuwa na haki ya kusitisha au kufunga akaunti yako kama tunaona ama tuna sababu ya kuamini kuwa unaweka pesa bila kuwa na nia ya kucheza/kubashiri. Unaweza tu kucheza/bashiri ukiwa na pesa kwenye akaunti yako.

3.2. Fedha za ziada (bonasi) zinaweza kuwekwa kwenye akaunti yako kama sehemu ya promosheni, uaminifu au kampeni nyingine za masoko. Fedha hizi haziwezi kutolewa moja kwa moja/ kulipwa, lakini lazima zitumike kufanya ubashiri. Kutegemeana na promosheni, pesa hizo zinaweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu baada ya kukidhi Vigezo na Masharti maalum kuhusiana na promosheni hiyo.

3.3. Unaweza, wakati wowote, kuingia kwenye akaunti yako na kupata tarifa ya miamala yote uliyofanya, kama vile amana, malipo ya ziada(bonasi), pesa uliyoshinda, pesa uliyotumia kubashiri na pesa ulizotoa. Endapo utagundua tatizo lolote, utapaswa mara moja kutoa taarifa kwa Kampuni kwa njia ya maandishi au kielektroniki. Tatizo hilo endapo likithibikika, litarekebishwa na Kampuni ndani ya muda mfupi iwezekanavyo bila gharama yoyote kwako.

3.4. Kutegemea na ufanyaji kazi wa mifumo yote sawasawa kama inavyotazamiwa, unaweza kutoa fedha kwenye akaunti yako ya Sportpesa. Kuna mifumo ya udhibiti na uhakiki kabla ombi la kutoa pesa halijashughulikiwa ambapo hatua hiyo ikikamilika utatumiwa ujumbe mfupi pamoja na namba ya uhakiki. Ukaguzi huu ni sehemu ya dhamira yetu endelevu ili kuhakikisha usalama wa fedha za wateja wetu. Maombi ya kutoa pesa ni lazima yafanyike ndani ya dakika kumi na tano (15) baada ya kupokea namba ya uhakiki ambapo baada ya hapo namba hiyo itapoteza uwezo wa kutumika tena. Gharama za utoaji fedha zitakazotozwa na huduma za kifedha (Mpesa, Airtel Money, Tigopesa, Halopesa, EzyPesa) zitakatwa kutoka kwenye akaunti ya mchezaji.

3.5. Utakapojaribu kutoa pesa ambayo umeingiza kwenye akaunti yako lakini haijatumika kubashiri, Kampuni yawezatoza ada ya kukuhudumia ya asilimia kumi (10%) wakati wa kutoa fedha hiyo. Na pia, endapo miamala hiii itaonekana kutia shaka, Kampuni itatoa taarifa juu ya jambo hilo kwenye mamlaka husika na mchezaji anaweza kupoteza fedha hizi.

3.5.1. Pale itakapowezekana, miamala yote halali ya kutoa pesa itafanyika kwenye akaunti ya malipo ambayo amana iliwekwa kihalali. Malipo ya kutoa pesa yanaweza kufanyika tu kwa jina la na kwa mwenye akaunti aliyesajiliwa. Kwa aina nyingi za malipo, kutoa pesa kunaweza kukafanyika kwa kufuata hatua za kiitifaki zilizoainishwa, kulingana na uwepo wa fedha za kutosha kwenye akaunti yako ya ubashiri. Hakuna kiwango cha mwisho kilichowekwa kwa ajili ya kutoa pesa kwa siku lakini maombi ya kutoa pesa hayapaswi kuzidi;

  • 3.5.1.1. ukomo uliowekwa na mtoa huduma wako wa simu ya kiganjani;
  • 3.5.1.2. kiasi kikubwa zaidi ya shilingi 20,000,000/=, ambayo itahitaji utaratibu maalum
  • 3.5.1.3. kwa maelezo kamili juu ya kila aina maalum ya malipo, tafadhali wasiliana na huduma kwa mteja.

3.5.2. Ikiwa wakati unaomba kutoa fedha kwenye akaunti yako amana yako itakuwa haijachezwa yote, Kampuni itakuwa na haki ya kukata ada kutoka kwenye akaunti yako ili kufidia gharama zote za wastani zinazohusiana na miamala yote miwili, kuweka na kutoa pesa. Pale itakapolazimu, tozo zihusianazo na ombi la kutoa pesa zaweza kupunguzwa.

3.5.3. Kama tutaingia gharama yoyote ya kurudisha pesa, kurudia muamala au gharama nyingine yoyote kuhusiana na akaunti yako, tutakuwa na haki ya kukukata fedha kufidia gharama hiyo.

3.5.4. Kampuni inaweza, wakati wowote, kukata fedha kwenye akaunti yako ili kufidia deni lolote unaloweza kuwa unadaiwa na Kampuni.

3.5.5. Endapo utaweza kuzifikia na kushiriki katika huduma zetu ukiwa nje ya Tanzania, utakuwa na wajibu wa kuzitaarifu mamlaka za kodi ama mamlaka zingine husika juu ya fedha ulizoshinda na ulizopoteza kwa mujibu wa sheria za nchi husika.

3.5.6. Michezo ya kubahatisha, kubashiri ama kamari yaweza kuwa kinyume cha sheria katika nchi uliko. Utakapojaribu kufanya muamala kwenye majukwaa yetu kutokea nchi ambazo ubashiri/michezo ya kubahatisha ni kinyume cha sheria, utafanya hivyo kwa ridhaa yako mwenyewe na Kampuni haitowajibika kwako ama kwa mtu yeyote kutokana na kitendo chako.

3.6. Kampuni itakuwa na haki ya kusitisha kwa muda muamala wako kwa minajili ya:

  • 3.6.1. kuhakiki utambulisho wako;
  • 3.6.2. kuhakiki mwenendo wa michezo yako;
  • 3.6.3. kufanya taratibu za kiusalama na nyingine kuhusiana na akaunti yako; na
  • 3.6.4. kuhakikisha kuwa zawadi zilizopatikana zinalipwa kwa mtu stahiki;

3.7. Endapo utahitaji kufunga akaunti yako, tafadhali wasiliana na kitengo cha huduma kwa mteja. Ikiwa kwa namna yoyote, akaunti yako itaonesha kuwa unadaiwa, maramoja deni hilo litapaswa kulipwa kwenye Kampuni, na akaunti yako haitositishwa mpaka pale deni hilo litakapokuwa limelipwa lote.

4. KANUNI ZA KUBASHIRI NA AINA ZA UBASHIRI
+

4.1. Tafsiri:

Katika kanuni hizi maneno yafuatayo yana maana kama ifuatavyo isipokuwa kama muktadha wake utahitaji maelezo mengine:

4.1.1. ‘Bashiri’ inamaanisha - kuweka fedha kwaajiri ya kutabiri matokeo ya tukio la kimchezo.

4.1.2. ‘Odds’ inamaanisha – pato kwenye fedha iliyochezwa iwapo utabiri uliofanywa kwenye bashiri utakuwa sawa sawa. Odds zinazolipwa ni zile zilizowekwa wakati ubashiri unafanyika na si vinginevyo.

4.1.3. 'Mteja' inamaanisha - mtu yeyote anaefanya ubashiri katika Kampuni.

4.1.4. 'Mtumiaji' inamaanisha - mtu yeyote anaetumia tovuti hii

4.1.5. 'BATILI' inamaanisha - kwa sababu moja au nyingine ubashiri haukubaliki na Kampuni. Katika mazingira kama haya, bashiri hii, au sehemu ya bashiri, hulipwa kwa odd ya 1.00. Zikiwa bashiri nyingi/mchanganyiko wa bashiri, matokeo yasiyokubalika hayatojumuishwa kwenye hesabu za (jumla) odds. Ikiwa ni bashiri moja, hii itamaanisha dau linarudishwa kwa mteja.

4.1.6. 'Muda kamili' (MK) inamaanisha - ule muda rasmi wa dakika 90 za mechi kukamilika, pamoja na muda wa ziada unaoongezwa na refa kufidia majeruhi kupata matibabu, kubadilishwa kwa wachezaji ama kupoteza muda kwa makusudi kunakofanywa na wachezaji (kipindi kijulikanacho pia kama dakika za majeruhi).

4.1.7. Muda kamili hautahusisha vipindi vya mapumziko vilivyopangwa (zile dakika 15 mara mbili za muda wa mapumziko), penalti n.k.

4.1.8. Kipindi cha kwanza (KK1) inamaanisha - pale dakika 45 za kwanza za mechi zinapokamilika pamoja na muda wa ziada unaoongezwa na refa kufidia majeruhi kupata matibabu, kubadilishwa kwa wachezaji ama kupoteza muda kwa makusudi kunakofanywa na wachezaji (inayojulikana pia kama dakika za majeruhi). Bashiri zilizofanywa Kipindi cha kwanza hushughulikiwa baada ya muda wa mwisho kuisha.

4.1.9. Zaidi/Chini ya 1.5 - Kipindi cha kwanza inamaanisha - UKIBASHIRI ZAIDI ya magoli 1.5 kufungwa, unashinda endapo bao 2 au zaidi zitafungwa. Ukibashiri CHINI ya magoli 1.5 kufungwa, unashinda endapo kuna goli 0 au goli 1 limefungwa.

4.1.10. Juu ya/Chini ya 2.5 inamaanisha - UKIBASHIRI ZAIDI ya magoli 2.5 kufungwa unashinda endapo mabao matatu au zaidi yatafungwa. UKIBASHIRI CHINI ya magoli 2.5, utashinda endapo mabao mawili au chini ya hapo yatafungwa kwa maana ya mmagoli 0,1 au 2.

4.1.11. Bao Sahihi inamaanisha – kubashiri idadi kamili ya mabao yatakayofungwa na kila timu ndani ya muda rasmi wa mchezo. Kwa madhumuni ya bashiri, mabao yakujifunga yanahesabika kwa niaba ya timu iliyofungiwa.

4.1.12. Bao sahihi - Kipindi cha kwanza inamaanisha - kubashiri idadi kamili ya mabao yatakayofungwa na kila timu wakati kipipindi cha kwanza kinaisha. Kwa madhumuni ya bashiri, mabao ya kujifunga yanahesabika upande wa timu yalikofungwa.

4.1.13. Timu zote mbili kufunga inamaanisha - bashiri ikiwa timu zote mbili zitafunga walau bao moja kila mmoja ndani ya Muda kamili wa mechi ama la.

4.1.14. Witiri /Shufwa inamaanisha - bashiri ikiwa jumla ya magoli katika mechi itakuwa witiri (1,3,5,7...) au shufwa (2,4,6,8...) ama la. Mabao 0 (sifuri) yatahesabiwa kama SHUFWA. Mabao ya kujifunga yatahesabika.

4.1.15. "Euro Handicap" 1:0 inamaanisha - bashiri matokeo pale timu ya nyumbani inapopewa faida ya goli 1 na hii kuongezwa kwenye mabao yao ya mwisho. Bashiri zitakamilishwa kwa kuongeza goli hilo kwenye magoli ya timu ya nyumbani baada ya mechi kukamilika.

4.1.16. "Euro Handicap" 0:1 inamaanisha - bashiri matokeo pale timu ya ugenini inapopewa faida na hii kuongezwa kwenye matokeo yao ya mwisho. Bashiri zitakamilishwa kwa kuongeza goli hilo katika idadi ya mabao ya timu ya ugenini baada ya mechi kukamilika.

4.1.17. Idadi kamili ya magoli inamaanisha - bashiri idadi kamili ya mabao yatakayofungwa ndani ya muda kamili.

4.1.18. Muda wa mapumziko/ Muda kamili inamaanisha - bashiri matokeo ya mechi katika vipindi vyote, wakati wa mwisho wa Kipindi cha kwanza na wa Muda kamili wa mechi.

4.1.19. Nafasi mbili inamaanisha - bashiri matokeo mawili kati ya matatu ya mechi kwa ubashiri mmoja.

Chaguzi zifuatazo zinapatikana:

  • 1 au X - Matokeo ni ama timu ya nyumbani kushinda au kutoka suluhu.
  • X au 2 - Matokeo ni ama suluhu au timu ya ugenini kushinda
  • 1 or 2 - Matokeo ni ama timu ya nyumbani kushinda au timu ya ugeni

4.2. Unaweza kubashiri endapo tu umejisajili kikamilifu na Kampuni na uthibitisho wa hilo kutumwa kwako.

4.3. Unaweza kubashiri pale tu unapokuwa na salio la kutosha kwenye akaunti yako. Bashiri/dau halitaidhinishwa endapo akaunti yako haina salio la kutosha.

4.3.1. Bashiri zote zinazokubalika na Kampuni ni za Muda kamili wa mechi, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo.

4.3.1.1. Kwa mechi zinazopangwa kumalizika ndani ya muda usio wa kawaida (mf. Dakika 60,80,au 120) kama inavyoelezwa na sheria za mashindano husika au kulingana na makubaliano ya pande zote mbili kabla ya mchezo kuanza, bashiri zote zinazokubalika zitalipwa baada ya kumalizika muda wa mchezo husika, kwa kadri itakavyokuwa, ikiwa ni pamoja na muda wa nyongeza utolewao na mwamuzi kwaajili ya kukamilisha mchezo (lakini haitohusisha muda wa ziada na mikwaju ya penalti), bila kujali kama muda wa mchezo umetangazwa nasi au la. Kifungu hiki chawezatumika, kwa mfano, wakati wa mechi au mashindano ya kirafiki.

4.3.1.2. Endapo mchezo utachezwa katika mfumo usio wa kawaida (mf. Vipindi vitatu au vinne), bashiri zote zinazofanywa wakati wa mapumziko zitabatilishwa lakini bashiri nyingine zote zinazokubalika zitalipwa kulingana na matokeo baada ya kumalizika kwa muda wa mchezo husika kama ilivyotafsiriwa katika kifungu hiki.

4.3.2. Bashiri yoyote itakayokubalika baada ya mechi kuanza italipwa kwa hiari ya Kampuni.

4.3.3. Endapo mechi imeahirishwa rasmi au vinginevyo, kufutwa, kuachwa, kukatishwa au kusitishwa, Kampuni itakuwa na haki ya kufuta mara moja bashiri zilizofanywa ndani ya saa 72 za kusitisha au kuahirishwa kwa mechi hiyo na kisha kurudisha hela za mteja.

4.3.3.1. Endapo mechi imeairishwa, kufutwa au kutelekezwa, kukatishwa au kusitishwa, ikiwa ni bashiri moja, bashiri itafanyiwa tathmini kama 'iliyoshinda' na odds 1.00. Hii itamaanisha kuwa mtumiaji atarudishiwa pesa kiasi cha dau lake.

4.3.3.2. Endapo mechi imeairishwa, kufutwa au kutelekezwa, kukatishwa au kusitishwa, ikiwa ni bashiri nyingi, mechi hiyo itakuwa na matokeo ya odd ya 1.00. Hii inamaanisha jumla ya odds itarekebishwa ipasavyo na bashiri hiyo bado inaweza kushinda, iwapo bashiri zingine zimeshinda pia.

4.3.4. Mechi zilizofutwa/kutelekezwa: mechi iliyofutwa/iliyotelekezwa itachukuliwa kuwa ni mechi ambayo imesitishwa kabla ya kukamilika kwa muda wake uliopangwa na ambayo haijachezwa mpaka mwisho.

4.3.4.1. Ikiwa ni bashiri moja, bashiri hiyo itakuwa batili baada ya masaa 24 kupita. Bashiri hii itafanyiwa tathmini kama 'imeshinda' kwa odd ya 1.00. Hii itamaanisha mtumiaji atapata pesa sawasawa na dau lake.

4.3.4.2. Ikiwa ni bashiri nyingi (multi bet), mechi husika itafanyiwa tathmini kama 'imeshinda' kwa odds ya 1.00. Hii itamaanisha kuwa jumla ya odds itarekebishwa ipasavyo na bashiri nyingi bado zitaweza kushinda iwapo bashiri zingine zinazoambatana nazo zitashinda pia.

4.3.5. Endapo kutakuwa na marudio ya mechi/kumalizia kiporo, kutolewa kwa ushindi wa mezani na vyombo husika ama maamuzi ya pamoja ya wahusika, yote haya hayatahesabika katika kuamua bashiri.

4.3.6. Pale ambapo mechi imetelekezwa, imekatishwa au imeahirishwa, kanuni zifuatazo zitatumika katika kulipa bashiri:

4.3.6.1. Kama bashiri imekamilika kabla ya kukatishwa, kutelekezwa au kuahirishwa kwa mechi, bashiri zitasimama na malipo kufanyika kama ilivyo tarajiwa.

4.3.6.2 Kama bashiri haijakamilika wakati wa mechi kukatishwa, kutelekezwa au kuahirishwa, bashiri zote zitakuwa batili.

4.3.6.3. Kama mechi itakatishwa, kutelekezwa au kuahirishwa wakati wa kipindi cha pili cha mechi, basi bashiri zote za kipindi cha kwanza zitasimama na malipo kufanyika kama ilivyotarajiwa.

4.3.6.4. Pale mechi itakapokatishwa, kutelekezwa au kuahirishwa lakini matokeo yake yakathibitika, bashiri itakubalika na malipo kufanyika kama ilivyotarajiwa

4.3.7. Bashiri Wakati Mechi Ikiendelea - endapo tutakuwa na sababu ya kuamini kuwa bashiri imefanywa baada ya matokeo kujulikana, au wakati tayari kuna tukio ambalo linampa faida zaidi mshiriki au tim iliyochaguliwa, (Mf. goli, kuonyeshwa kadi nyekundu mchezaji wa timu nyingine n.k.), tutakuwa na haki ya kubatilisha bashiri, iwe imeshinda au imeshindwa.

4.3.8. Ikiwa, kwa sababu yoyote ile, tutashindwa kuhakikisha matokeo katika eneo/soko fulani (Mf. kutokana na kupotea kwa picha mubashara), bashiri zote zitakuwa batili, isipokuwa tu kama malipo ya bashiri hiyo yatakuwa yamekwishakuamuliwa.

4.3.9 Endapo mteja atafanya tabiri yenye utata, Kampuni ina haki ya kugawa kiwango cha dau kilichowekwa katika uwezekano wa matokeo. Ikiwa hili halitowezekana, tuna haki ya kubatilisha bashiri yote. Vyovyote iwavyo, maamuzi ya Kampuni ndiyo yatakuwa maamuzi ya mwisho.

4.4. Kwa kufanya ubashiri, unathibitisha nia yako ya kukamilisha muamala huo. Bashiri ikishakamilika, itatawaliwa na vigezo na mashartikwa vinavyotumika wakati ukifanya ubashiri huo.

4.4.1. Kampuni haitawajibika kwa makosa ya kiuandishi, uhamishaji wa taarifa, na/au makossa ya kitathmini. Na haswa, Kampuni itakuwa na haki ya kurekebisha makosa ya wazi–hata baada ya tukio–kwa kurekebisha odds za kubashiri na/au tathmini ya matokeo ya bashiri (Mf. makosa yanayohusu odds, timu, inayohusu ama tukio) au kutangaza bashiri zilizoathiriwa na makossa hayo kuwa batili. Kampuni pia haitohusika kwa lolote kuhusiana na usahihi, ukamilifu au uthabiti wa habari inayotolewa, mfano magoli mubashara na jumbe za matokeo zinazotumwa kwa barua pepe au ujumbe mfupi wa maneno (SMS). Dau ni lile tu lililothibitishwa na kuingizwa katika kumbukumbu ya kampuni. Ikiwa tukio/soko lenye makosa limefutwa, bashiri zote zitakuwa batili na zitatathminiwa kanakwamba zimeshinda kwa odds ya 1.00.

4.5. KUKUBALI NA KUSITISHA BASHIRI

4.5.1. Ubashiri uliofanywa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno utachukuliwa kama umefanyikaa mara tu mchezaji atakapopokea ujumbe wa kukubali kutoka kwenye Kampuni. Ukisha kubaliwa, ubashiri uliofanywa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno wawezasitishwa tu ndani ya dakika 10 (kumi) toka ufanyike. Usitishwaji utakubaliwa ikiwa tu mechi haijaanza ndani ya hizo dakika kumi.

4.5.2. Bashiri iliyofanywa kwa njia ya mtandao wa Kampuni itachukuliwa kuwa imefanyika mara tu ujumbe wa uthibitisho utakapoonekana kwenye kioo. Mara tu bashiri hiyo ikishakubalika, haiwezekani tena kuisitisha.

4.5.3. Kampuni itakuwa na haki ya kuzikataa bashiri/dau zote au sehemu ya bashiri/dau hizo kwa kadri itakavyoona inafaa yenyewe ikiwa kuna shida ya kitaalam, kuna udanganyifu, njama za kubeti ama kubashiri tukio ambalo matokeo yanajulikana tayari.

4.5.4. Tunakubali bashiri/dau linalowekwa kwa njia ya simu ya kiganjani ama tovuti ya Kampuni pekee. Bashiri/madau hayapokelewi kwa njia nyingine yoyote ile (posta, barua pepe, faksi nk.) na pale bashiri hizo ama madau yatakapopokelewa yatakuwa yasiyokubalika na batili.

4.5.5. Ni wajibu wa mteja kuhakikisha maelezo ya bashiri/dau lake ni sahihi.

4.5.6. Bashiri zitashughulikiwa kufuatana na zilivyopokelewa.

4.6. Unakubali kuwa wakati unafanya ubashiri wako, hukuwa ukijuamatokea matokea ya matukio husika. Hauruhusiwi kubashiri katika matukio ambayo unahusika moja kwa moja ama unaweza kupata taarifa za ndani. Pale kutakapokuwa na tuhuma juu ya kula njama, /udanganyifu ama kitendo chochote kinachopelekea uvunjifu wa kanuni hii, Kampuni ina haki ya kubatilisha ubashiri na kukataa ushindi wako. Kampuni pia ina haki ya kuchukua hatua zaidi kulinda maslahi yake halali kwa kuzingatia sheria za nchi, sheria za kimataifa pamoja na kanuni. Vitendo vyovyote vinavyotia shaka vyaweza kuwasilishwa kwenye vyombo husika kwa hatua zaidi ili kulinda na kudumisha uadilifu wa michezo ya ubashiri.

4.7. Wakati wowote mchezaji atakapofanya zaidi ya ubashiri mmoja kwenye tukio moja, kila dau litahesabika kama ubashiri tofauti. Orodha ya bashiri zote, hali zao na maelezo zaidi inapatikana kwenye tovuti ya Kampuni.

4.8. Kampuni ina haki ya kutamka bashiri zote kwenye tukio fulani kuwa batili endapo bashiri hizo yaonekana zinatoka kwenye kundi la wachezaji wanaoonekana kuwa na taarifa juu ya matokeo ya tukio hilo (ubashiri wa genge la watu).

4.9. Mtu yeyote au kundi la watu wanaoaminika kufanya kazi pamoja wakiathiri promosheni na ofa nyingine, watafungiwa akaunti zao mara moja. Aidha, miamala (bashiri) husika haitachangia katika promosheni yoyote au mahitaji ya ofa za bonasi.

4.10. Kampuni pia ina haki ya kurudisha bonasi yoyote iliyotolewa kwako, na kupunguza kiasi hicho kutoka kwenye dau la ubashiri, endapo utagundulika kutumia vibaya mfumo kama inavyobainishwa kwenye masharti haya.

4.11. Iwapo Kampuni itaamua kufunga akaunti yako kwa sababu yoyote zile, bashiri ambazo tayari zimefanyika na kukubalika kwa mujibu wa Kanuni pamoja na taratibu za ubashiri, hazitabatilishwa, na utalipwa ushindi wako kama umeshinda. Endapo maswali ya kiusalama yataibuka kuhusiana na akaunti yako, Kampuni ina haki ya kubatilisha miamala hiyo (bashiri) kwa mujibu wa sheria na tmisingi ya udhibiti, kubakia na kutumia haki yake ya kushikilia kiasi chochote kwenye ushindi wako na kukupatia kiasi kinachobakia ukitoa gharama zozote husika.

4.12. Unapofanya ubashiri, unathibitisha kuwa umesoma, umeelewa na kukubaliana kikamilifu na Kanuni zote pamoja na taratibu za ubashiri kuhusiana na bashiri zinazotolewa na Kampuni kama ilivyoelezwa kwenye Tovuti ya Kampuni na vyombo vingine vyote vya habari/majukwaa ya kielektroniki.

4.13. Malipo juu ya bashiri za odds zisizobadilika huhesabiwa kwa kuzidisha dau la awali kwa desimali za odds zilizotolewa kabla. Matokeo ya hesabu hii yanahusisha pia dau la awali ambalo hurudishwa kwa bashiri zote zilizofanyika kwa pesa halisi (yaani isiyohusisha bashiri zilizofanywa bila pesa).

4.14. Ikiwa umeshinda bashiri ulioifanya: Ujumbe mfupi wa maneno utatumwa kwenye namba yako ukikujulisha kuwa umeshinda na ukikuonyesha salio la akaunti yako.

4.15. Pesa ya ushindi italipwa moja kwa moja kwenye akaunti yako baada ya matokeo ya mwisho kuthibitika. Mabadiliko yoyote ya matokeo yatakayofanywa baadae, mf. taratibu za kinidhamu (kutumia dawa) au kuingilia kati kwa vyombo vinavyosimamia matukio hayo ambavyo hupelekea matokeo yale kufanyiwa mabadiliko hayatohesabika kwa lengo la kuamua matokeo ya bashiri. Hata hivyo, Kampuni itakuwa na haki ya kuukataa ushindi wowote iwapo kuna uchunguzi juu ya tukio lililosababishwa na tuhuma za vitendo vya jinai vinavyowezakuwa vimeathiri matokeo ya tukio. Ikiwa uchunguzi utabaini makossa yoyote, Kampuni itakuwa na haki ya kubatilisha bshiri zote zinazohusika.

4.16. Endapo bashiri nyingi (Mf. mara mbili, mara tatu, mara nne, nk) zimefanywa katika mfumo wa mchanganyiko wa mafungu kupitia kwenye mkeka (Mf.3 X mara mbili, 2 X mara tatu), bashiri zote zitakazo wasilishwa kwa mfumo huu zitalipwa mara baada ya tukio la mwisho katika mchanganyiko kukamilika. Kwa mfano, iwapo utachagua masoko matatu katika mkeka wako na kuweka mchanganyiko wa mbilimbili mara tatu wa kiwango cha juu cha mwisho, mbilimbili zote tatu hazitalipwa mpaka soko la mwisho litakapo kamilika*.

*Baadhi ya mechi zinaweza kuwa na Muda kamili (MK) wa dakika themanini (80) kwa mujibu wa kanuni za FIFA, mechi hizo ni pamoja na; Chini/16, Chini/17, Michuano ya wanawake nk*

4.17. Dau la juu na la chini katika ubashiri:

  • 4.17.1. Kiwango cha chini cha kiasi cha kubashiri: Kiwango cha chini cha kiasi cha kubashiri kwa bashiri moja/bashiri nyingi ni Sh. 100/=
  • 4.17.2. Kiwango cha juu cha kiasi cha kubashiri: Kiwango cha juu cha kiasi cha kubashiri kwa bashiri moja / nyingi ni Sh. 500,000/=
  • 4.17.3. Kiwango cha juu cha ushindi wa bashiri moja: kiasi cha ushindi kwa Bashiri Moja si zaidi ya Sh. 5,000,000/=
  • 4.17.4. Kiwango cha juu cha ushindi wa bashiri nyingi: kiasi cha juu cha ushidi kwa bashiri nyingi si zaidi ya Sh. 25,000,000/=
  • 4.17.5. Kiwango cha juu cha jumla cha ushindi (kiwango cha juu cha malipo): kiwango cha juu cha kiasi cha ushindi kwa mteja mmoja kwa siku hakizidi Sh. 30,000,000/=

4.18. Viwango vya ubashiri vilivyotajwa hapo juu kwenye 4.17 vinaweza kubadilika kulingana na maamuzi ya Kampuni. Hauruhusiwi kufanya ubashiri au kujaribu kufanya ubashiri kwa vima ambavyo ni chini au Zaidi ya vilivyowekwa.

4.18.1. Wachezaji wanaweza kuomba kuweka ubashiri wa juu zaidi ya kiwango kilichowekwa na makubaliano ya maandishi yanaweza kuingiwa ili ktekeleza hilo. Tafadhali wasiliana na kitengo chetu cha huduma kwa mteja kuanzisha mchakato huu.

4.18.2 Kiwango cha juu cha malipo kwa akaunti yoyote ni Sh. 30,000.000/=. Bashiri inakubaliwa kwa misingi kwamba ni uwekezaji wa mteja mmoja tu na kwamba ni kiwango cha juu cha fedha anachoweza kushinda (mbali na dau) kwa siku bila kujali dau.

4.19 Bashiri zote na dau zitapaswa kufuata kikamilifu vipengele vyote vinavyohusiana na viwango vya ubashiri (ikiwa ni pamoja na kiwango cha juu cha ushindi) katika kanuni hizi na:

  • 4.19.1 Kampuni ina haki ya kusitisha na/au kufuta ubashiri/dau lolote wakati wowote ikiwa kuna shida ya kitaalam, kuna udanganyifu, njama za kubeti ama kubashiri tukio ambalo matokeo yanajulikana tayari.Bashiri/uwekaji dau ama mchezo ukisitishwa, bashiri yoyote itakataliwa. Kampuni pia ina haki ya kusitisha kufanyika kwa ubashiri katika eneo lolote ndani ya nchi wakati wowote bila ya taarifa.
  • 4.19.2. Ushindi kutoka bashiri zilizolipwa huongezwa kwenye Salio la akaunti yako ya kubashiri. Fedha yoyote ya ushindi iliyoingizwa kwenye akaunti kimakosa haipaswi kutumika na Kampuni ina haki ya kubatilisha miamala yoyote inayohusiana na fedha hizo na/au kubatilisha utoaji wa fedha hizo kutoka kwenye akaunti yako na/ama kurudisha muamala, aidha wa wakati huo au wa kabla ya hapo.
  • 4.19.3. Kwa matukio ambayo hakuna muda rasmi wa kuanza uliotangazwa, muda wa kuanza uliotangazwa utachukuliwa kuwa ndio muda rasmi wa kuanza. Ikiwa kwa bahati mbaya bashiri yoyote itakubaliwa baada ya tukio au mechi kuanza, bashiri itaendelea endapo tu matokeo ya mwisho hayajulikani, na kwamba hakuna mshiriki/timu iliyopata faida yoyote kubwa (Mf. goli, kutolewa nje kwa kadi nyekundu, nk) wakati bashiri inafanyika. Endapo matokeo ya tukio/soko yanajulikana, Kampuni ina haki ya kubatilisha bashiri, kushinda au kupoteza. Migogoro juu ya muda wa ubashiri itashughulikiwa kwa kutumia kumbukumbu ya muamala. Saa zote zilizosemwa kwenye huduma za Simu, Tovuti na vyombo vingine vyote/majukwaa ya kielektroniki na/au inayoelezwa na wafanyakazi wa Kampuni ni zile za majira ya Afrika Mashariki isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo.

4.20. Kampuni haitawajibika kwa makossa ya uwekji au ya uhamishaji wa taarifa. Kampuni ina haki ya Kurekebisha makosa ya wazi hasa katika uwekaji wa odds za ubashiri kwa mfano kuchanganywa kwa odds au matokeo, timu, nk.

4.21. Kampuni haitawajibika kwa usahihi au ukamilifu wa habari zinazotolewa.

4.22. Kampuni haitawajibika kwa uthabiti wa magoli mubashara, takwimu na matokeo ya kati kwa bashiri mubashara.

4.23. Aina za bashiri

4.23.1. Bashiri moja

Bashiri moja ndio aina ya ubashiri rahisi zaidi. Unatabiri matokeo, unaweka bayana dau unalopendelea na unaweka bashiri. Kama utabiri wako utakuwa sahihi, unashindaubashiri huo. Kiwango unachoshinda kinapatikana kwa kuzidisha odds na dau.

4.23.1.1. Bashiri moja kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS)

Hapa unachagua mechi unayobashiria kwa kutumia kitambulisho mchezo/mechi (ID). Unatuambia utabiri wako kwa kuuongeza kwenye kitambulisho mchezo/mechi. Ushindi wa nyumbani ni 1, ushindi wa ugenini ni 2, na suluhu ni X. Utuambia ni kiasi gani unataka kuweka kama dau kwa kuongeza dau lako mwishoni mwa bashiri. Sh. 2,000 ni 2,000. Kwa hiyo, kubashiri Sh. 2,000 kwa mechi yenye kitambulisho mchezo 6981, kutabiri ushindi wa nyumbani, unatuma ujumbe huu mfupi wa maneno 6981 #1#2000 kwa nambari yetu fupi.

Kisha Kampuni itatuma ujumbe mfupi wa maneno wenye uthibitisho kwenye namba yako ya simu ya kiganjani iliyosajiliwa, kuthibitisha ubashiri wako na uwezekano wa kushinda (ushindi unahesabika kwa kuzidisha odds na dau k.m.f 2.36×100=236).

Unaweza kufuta bashiri moja iliofanywa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno ndani ya dakika kumi baada ya kubashiri, lakini vyovyote iwavyo, isiwe baada ya mechi kuanza.

Kufuta bashiri moja iliyowekwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno unahitaji tu kutuma ujumbe wenye neno 'futa' ukifuatiwa na alama hii # na kitambulisho cha bashiri kwenda namba fupi ya Kampuni 15888 mf. Futa#6918. Utapokea ujumbe mfupi wa kuthibitisha kufutwa kwa ubashiri wako, mf. BET ID 6918 imefutwa. Sh. 2,000 imerudishwa kwenye akaunti yako ya M-PESA. Salio lako la M-PESA ni Sh. 38,193.

4.23.1.2. BASHIRI MOJA KUPITIA TOVUTI YA KAMPUNI

Waweza pia ukafanya bashiri moja kupitia tovuti ya Kampuni www.sportpesa.co.tz.

Tovuti ya Kampuni ni rahisi sana kuitumia na unachohitaji kufanya ni kufuata maelekezo kufika kwenye mchezo unaokufurahisha kisha bofya timu unayotaka ishinde ndani ya dakika 90 na mkeka wa kubashiri utafunguka. Kisha unaweka kiasi cha fedha unachotaka kubashiri. Ukishakubaliwa, jiandikishe. Kukamilisha kuweka bashiri yako hakikisha unabonyeza kwenye 'WEKA BASHIRI'. Ujumbe wa uthibitisho utaonekana kwenye kioo cha tovuti kukujulisha kuhusu maelezo ya ubashiri wako na kitambulisho cha bashiri moja, Mf. Umeweka Bashiri Moja ID6918 kwa Sh. 1000. Makisio yako ya ushindi ni Sh. 2360. Salio lako la M-Pesa ni Sh. 37,193.

Mara baada ya kubashili kwa njia ya tovuti ya Kampuni, bashiri moja haitaweza kufutwa kwenye tovuti. Hivyo, lazima uhakikishe kwamba una nia ya kufanya muamala wa bashiri kabla ya kubonyeza kitufe cha uthibitisho. Hata hivyo, bado unaweza ukafuta ubashiri wako kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno ndani ya dakika kumi baada ya kuiweka, lakini sio baada ya mechi kuanza. Katika kufanikisha hili, unahitaji kutuma ujumbe kutoka kwa namba yako ya simu ya kiganjani iliyosajiliwa na SportPesa kwa kuandika maneno ‘futa’ ikifuatiwa na alama ya # na kitambulisho cha bashiri kwa namba ya Kampuni 15888. Kisha ujumbe wa kuthibitisha kufutwa kwa bashiri yako utatumwa kwako.

4.23.2 BASHIRI NYINGI

Ikiwa tabashiri kuanzia mechi 2 na zaidi, moja kwa moja ubashiri wako utanyeshwa kama bashiri nyingi. Jumla ya odds inapatikana kwa kuzidisha odds za chaguzi mojamoja. Tafadhali tambua kuwa hautolipwa chochote kwenye bashiri nyingi mpaka pale bashiri zako zote ulizochagua zitakapokuwa sahihi. Kwa aina hii ya ubashiri, unaweza kufanya hadi chaguzi ishirini.

Mfano wa ubashiri huu wawezakuwa: Man Untd kushinda (1.35), Arsenal kushinda (1.75), Real Madrid kushinda (2.00). Kujua unachowezakushinda unazidisha tu kiasi kilichotajwa kwaajili chaguo, 1.35 X 1.75 X 2.00 = 4.72. Hii inamaanisha endapo chaguzi zako tatu zitashinda, utashinda 4.72 mara dau lako.

4.23.2.1. BASHIRI NYINGI KUPITIA UJUMBE MFUPI WA MANENO (SMS)

Tuma ujumbe mfupi wa maneno kwa namba yetu fupi, mfuatano wa kila namba ya utambulisho (ID) wa mchezo, utabiri wako kisha kiasi unachobashiri kama inavyooneshwa hapa chini: “1234#2#4534#1#7180#1#135”, ambapo 1234 ni kitambulisho cha mchezo, 1 ni utabiri, 4534 ni kitambulisho cha mchezo, 1 ni utabiri, 7180 ni kitambulisho cha mchezo, 1 ni utabiri na 135 ni kiasi cha fedha cha ubashiri.

Utapokea uthibitisho wa ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwenye Kampuni ukiwa na maelezo yote ya ubashiri ulioufanya.

Unaweza kufuta Bashiri Moja uliyofanya kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno ndani ya dakika kumi baada ya kuweka bashiri, lakini sio baada ya mechi kuanza.

Kufuta ubashiri mwingi kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno unahitajika kutuma neno ‘futa’ ikifuatiwa na alama ya # na kitambulisho cha ubashiri kwa namba fupi ya Kampuni 15888; Mf. Futa#7687.

Ujumbe wa kuthibitisha kufuta ubashiri wako utarudishwa kwako. Mf. BET ID 7687 imefutwa. Sh. 1350 imerudishwa kwenye akaunti yako ya M-PESA. Salio lako la M-PESA: Sh. 37,193.

4.23.2.2. Bashiri Nyingi kwa njia ya tovuti ya Kampuni

Pia unaweza kufanya bashiri nyingi kupitia tovuti ya kampuni (www.sportpesa.co.tz) .

Tovuti ya Kampuni ni rahisi sana kuitumia na unachohitaji kufanya ni kufuata maelekezo kufika kwenye mchezo unaokufurahisha kisha bofya timu unazotaka zishinde ndani ya dakika 90 na mkeka wa kubashiri utafunguka. Kisha unaweka kiasi cha fedha unachotaka kubashiri. Ukishakubaliwa, jiandikishe. Kukamilisha kuweka bashiri yako hakikisha unabonyeza kwenye WEKA BASHIRI. Ujumbe wa uthibitisho utaonekana kwenye kioo cha tovuti kukujulisha kuhusu maelezo ya ubashiri wako na namba ya utambulisho wako. Mf. Umeweka Bashiri Nyingi ID 7687 kwa Sh. 1350. KIASI UNACHOWEZA KUSHINDA Sh. 3976. Salio lako la M-PESA ni: Sh. 37,958.

Mara baada ya kufanywa kwa njia ya tovuti ya Kampuni, Bashiri Nyingi haitaweza kufutwa kwenye tovuti. Kwa hiyo, lazima uhakikishe kuwa una nia ya kufanya muamala wa ubashiri kabla ya kubonyeza kitufe cha uthibitisho. Hata hivyo, bado unaweza kufuta ubashiri wako kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno ndani ya dakika kumi baada ya kuufanya, lakini sio baada ya mechi kuanza. Ili kulitekeleza hili, unahitaji tu kutuma ujumbe kutumia namba yako ya simu ya mkononi iliyosajiliwa na SportPesa kwa kuandika maneno ‘futa’ ikifuatiwa na alama ya # na namba ya utambulisho wa bashiri (Bet ID) kwa namba fupi ya Kampuni 15888.

4.23.2.3. BONASI YA BASHIRI NYINGI

4.23.2.3.1. Sportpesa yaweza, kulingana na matakwa yake yenyewe, na kwa namna itajavyoona inafaa, kutoa bonasi kwenye bashiri nyingi.

4.23.2.3.2. Odds zinazozidi 1.29 pekee zitakuwa na uhalali wa kushiriki kwenye bonas.

4.23.2.3.3. Bonas itahesabiwa kutokana na ushindi halisi

4.23.2.3.4. Mteja atalazimika kufanya walau chaguzi 3 ili aweze kuingia kwenye kapu la bonas ya bashiri nyingi.

4.23.2.3.5. Ikiwa bashiri nzima au chaguo sahihi itasitishwa, batilishwa au kutolewa, bonasi ya bashiri nyingi itahesabiwa upya

4.23.2.3.6. Bonasi ya kuanzia unayoweza kushinda itahesabiwa kabla hujaweka bashiri.

4.23.2.3.7. Promosheni ni kwaajili ya burudani tu na inatolewa kwa utashi na matakwa pekee ya Sportpesa. Haitoi haki yoyote kwa mteja yoyote na Sportpesa yaweza kuiondoa, kuifuta, kuisitisha kwa muda ama kuondoa matumizi yake kabisa muda wowote na bila taarifa yoyote. Ikiwa mteja yeyote atapatikana akitumia vibaya promosheni hii, Sportpesa itakuwa na haki kuondoa bonasi yoyote na kumfungia mteja husika kushiriki promosheni yoyote itakayoandaliwa. 

4.23.3.1 JACKPOT

1. Jackpot inatokana na matukio kumi na tatu (13) ya mchezo wa mpira wa miguu ayochaguliwa kabla.

2. Kiwango cha fedha cha jackpot kitabadilika kila wiki.

3. Kiasi cha fedha cha jackpot kinagawanywa kwa usawa miongoni mwa washindi wote wa jackpot.

4. SportPesa ina haki ya kuzuia 90% ya mgao wa ushindi mpaka pale sherehe ya kutunuku ushindi itakapofanyika

5. Kwa tuzo kubwa zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni Mia Mbili (Tsh. 200,000,000/=) kampuni ina  haki ya kulipa kiasi chochote kwa awamu sita sawa.

6. SportPesa ina haki, isipokuwa kama inakatazwa na sheria, kutumia majina, rekodi za redio, video au picha za mshindi, kwa madhumuni ya kampeni na kama njia ya kujitangaza.

7. Washindi watatakiwa kufika ofisi za Sportpesa wakiwa na vitambulisho vyao kabla ya malipo yoyote. Sportpesa ina haki ya kuthibitisha, kupitia vyombo husika, kitambulisho chochote kitakacholetwa kabla ya kufanya malipo yoyote.

8. Kama sehem ya taratibu za malipo haya, washindi watatakiwa kutoa uthibitisho wowote unaokubalika juu ya utambulisho wao kabla malipo yoyote hayajafanyika.

9. Ikiwa mchezo wa jackpot umefutwa, droo rasmi kwa umma itafanyika baada ya masaa 72 kutoka ule muda wa kufutwa, ili kuamua matokeo ya mechi iliyopotea.

10. Kipindi cha kudai tuzo ni siku saba (7) ambapo ikishindikana SportPesa inaweza kuitaifisha zawadi hiyo, isipokuwa kama kipindi hicho kitaongezwa, kwa hiari pekee ya SportPesa.

11. Endapo michezo mitatu au zaidi imefutwa, kukatishwa, kuachwa, kusitishwa ama imeahirishwa, Sportpesa inaweza, kwa namna itakavyoona inafaa, ikafuta Jackpot na kurudisha dau lililowekwa ndani ya saa 72 baada ya ufutwaji huo.

12. Kima cha bashiri ya jackpot ni Shilingi za Tanzania Elfu Moja Tu (Sh. 1000.00).

4.23.3.2. BONASI YA JACKPOT

  1. Wachezaji wa jackpot wanastahili kupata zawadi za ziada (bonasi), kama vile ziada ya jackpot.
  2. Kiwango cha fedha cha bonasi ya jackpot kitaamuliwa na Sportpesa kwa hiari yake pekee.
  3. Bonasi ya jackpot itakuwa ni kwaajili ya wachezaji wenye utabiri sahihi kwa seti ya mechi 13 ya jackpot husika ya kila wiki kama ifuatavyo:
    1. Tabiri sahihi kumi na mbili (12) kati ya michezo kumi na tatu (13)
    2. Tabiri sahihi kumi na moja (11) kati ya michezo kumi na tatu (13)
    3. Tabiri sahihi kumi (10) kati ya michezo kumi na tatu (13)
  4. Kiasi cha fedha cha bonasi kitatofautiana kati ya matabaka mbali mbali.
  5. Bonsi ya jackpot itagawanywa sawa sawia miongoni mwa washindi wa bonasi ya jackpot katika tabaka husika.
  6. Endapo mechi tatu (3) au zaidi zimefutwa, katishwa, achwa, sitishwa au ahirishwa, Sportpesa yaweza, kadri inavyoona inafaa, ikafuta bonasi ya jackpot na kurejesha dau lililowekwa ndani ya saa 72 baada ya ufutwaji huo.

4.23.3.3. JACKPOT YA BASHIRI UNGANIFU

  1. Jiongezee faida zaidi na jackpot ya bashiri mbili kwa pamoja (bashiri pacha) inayokuruhusu kufanya ubashiri kwa kufanya chaguzi mbili katika mchezo mmoja, kwa hadi michezo saba kutoka katika orodha ya michezo kumi na tatu ya jackpot katika bashiri moja ya jackpot.
  2. Kadri unavyofanya bashiri mbili kwa pamoja mara nyingi, ndivyo nafasi ya kushinda inavyoongezeka. Mahesabu ya idadadi ya bashiri pacha ni sawa na 2n (ambapo n ni idadi ya bashiri pacha). Kwa mfano bashiri pacha nne (4) itakuwa sawa na 16(2*2*2*2) bashiri za jackpot moja.
  3. Gharama ya bashiri pacha inahesabiwa ifuatavyo: idadi ya miunganiko (2n, ambapo n ni idadi ya pacha )* Sh. 2,000. Kwa mfano kwa bashiri pacha nne (4) za jackpot, gharama itahesabiwa kama 2*2*2*2=16 miunganiko *2,000/- = 32,000/- kwa bashiri iliyowekwa.
  4. Bashiri pacha yawezakuwa kwa kiwango cha chini na pacha moja na hadi ukomo wa pacha saba kutoka katika michezo kumi na tatu (13) ya jackpot katika bashiri ya jackpot.
  5. Kiwango cha juu cha jackpot ya bashiri pacha kinaundwa na seti tofautitofauti za jackpot moja mia moja ishirini na nane (128) za tabiri 13 zilizowekwa katika bashiri moja ya Jackpot.
  6. Jumla ya gharama ya kiwango cha juu cha jackpot ya bashiri pacha itakuwa elfu kumi na mbili na mia nane, kama ifuatavyo: (chaguzi za bashiri 128*2,000 Sh. kwa kila bashiri = Sh. 256,000)
  7. Endapo utaweka pacha unganifu n, kila seti moja ya 2n ya tabiri 13 inachukuliwa kama bashiri binafsi na inaweza kushinda VYOTE vifuatavyo:
    1. The Jackpot;
    2. Bonasi kwa tabiri sahihi kumi na mbili (12);
    3. Bonasi kwa tabiri sahihi kumi na moja (11)
    4. Bonasi kwa tabiri sahihi kumi (10);
  8. Endapo michezo mitatu au zaidi imefutwa, katishwa, achwa, sitishwa ama ahirishwa, Sportpesa yaweza, kwa kadri itakavyoona inafaa, ikafuta bashiri za jackpot unganifu na kurudisha dau lililowekwa ndani ya masaa 72 ya kufutwa.

4.23.3.4. SUPA JACKPOT

1. Sportpesa inayo furaha kutambulisha kwako jackpot yake mpya iitwayo "Supa Jackpot". Jackpot hii imegawanyika katika vipengele vinne kama ifuatavyo:

a. 17/17. Chinini ya kipengele hiki, mteja hubashiri matokeo ya michezo 17. Ikiwa matokeo ya michezo yote yatakuwa kama ilivyobashiriwa, mteja atakuwa ameshinda jackpot. Sportpesa inaweza, kwa utashi wake pekee na kwa kadri itakavyoona inafaa, kutoa bonasi kwa wateja ambao watapatia ubashiri wa michezo mingi kutegemeana na ukaribu wa kushinda jackpoti. Kiwango cha awali cha jackpot ni Sh. 1,000,000,000.00 (Yaani shilingi za Tanzania Bilioni Moja).

b. 16/16. Chinini ya kipengele hiki, mteja hubashiri matokeo ya michezo 16. Ikiwa matokeo ya michezo yote itakuwa kama ilivyobashiriwa, mteja atakuwa ameshinda jackpot. Sportpesa inaweza, kwa utashi wake pekee na kwa kadri itakavyoona inafaa, kutoa bonasi kwa wateja ambao watapatia ubashiri wa michezo mingi kutegemeana na ukaribu wa kushinda jackpoti. Kiwango cha awali cha jackpot ni Sh. 750, 000,000.00 (Yaani shilingi za Tanzania Milioni Mia Saba Hamsini).

c. 15/15. Chinini ya kipengele hiki, mteja hubashiri matokeo ya michezo 15. Ikiwa matokeo ya michezo yote itakuwa kama ilivyobashiriwa, mteja atakuwa ameshinda jackpot. Sportpesa inaweza, kwa utashi wake pekee na kwa kadri itakavyoona inafaa, kutoa bonasi kwa wateja ambao watapatia ubashiri wa michezo mingi kutegemeana na ukaribu wa kushinda jackpoti. Kiwango cha awali cha jackpot ni Sh. 500, 000,000.00 (Yaani shilingi za Tanzania Milioni Mia Tano).

d. 14/14. Chinini ya kipengele hiki, mteja hubashiri matokeo ya michezo 14. Ikiwa matokeo ya michezo yote itakuwa kama ilivyobashiriwa, mteja atakuwa ameshinda jackpot. Sportpesa inaweza, kwa utashi wake pekee na kwa kadri itakavyoona inafaa, kutoa bonasi kwa wateja ambao watapatia ubashiri wa michezo mingi kutegemeana na ukaribu wa kushinda jackpoti. Kiwango cha awali cha jackpot ni Sh. 300, 000,000.00 (Yaani shilingi za Tanzania Milioni Mia Tatu).

e. 13/13. Chinini ya kipengele hiki, mteja hubashiri matokeo ya michezo 13. Ikiwa matokeo ya michezo yote itakuwa kama ilivyobashiriwa, mteja atakuwa ameshinda jackpot. Sportpesa inaweza, kwa utashi wake pekee na kwa kadri itakavyoona inafaa, kutoa bonasi kwa wateja ambao watapatia ubashiri wa michezo mingi kutegemeana na ukaribu wa kushinda jackpoti. Kiwango cha awali cha jackpot ni Sh. 200, 000,000.00 (Yaani shilingi za Tanzania Milioni Mia Mbili).

2. Kanuni zinazotumika kwenye jackpot ya kawaida zitatumika pia kwenye Supa Jackpot isipokuwa kama kanuni hizi zitaeleza vinginevyo. Ikiwa kutatokea msigano ama utofauti kati ya kanuni hizi na kanuni zinazotumika kwenye jackpot ya kawaida, kanuni hizi zitachukua nafasi.

4.23.3.3. SUPA JACKPOT YA BASHIRI UNGANIFU PACHA

1. Jiongezee faida zaidi na Supa jackpot ya bashiri mbili kwa pamoja (bashiri pacha) inayokuruhusu kufanya ubashiri kwa kufanya chaguzi mbili katika mchezo mmoja, kwa hadi michezo kumi kutoka katika orodha ya michezo kumi na saba ya supa jackpot katika bashiri moja ya supa jackpot.

2. Kadri unavyofanya bashiri mbili kwa pamoja mara nyingi, ndivyo nafasi ya kushinda inavyoongezeka. Mahesabu ya idadadi ya bashiri pacha ni sawa na 2n (ambapo n ni idadi ya bashiri pacha). Kwa mfano bashiri pacha kumi (10) itakuwa sawa na 1024(2*2*2*2*2*2*2*2*2*2) bashiri za supa jackpot moja.

3. Ghrama ya bashiri pacha inahesabiwa ifuatavyo: idadi ya miunganiko (2n, ambapo n ni idadi ya pacha )* Sh. 1,000. Kwa mfano kwa bashiri pacha kumi (10) za supa jackpot, gharama itahesabiwa kama 2*2*2*2*2*2*2*2*2*2=1024 miunganiko *1,000/- = 1,024,000/- kwa bashiri iliyowekwa.

4. Bashiri pacha yawezakuwa kwa kiwango cha chini na pacha moja na hadi ukomo wa pacha kumi kutoka katika michezo kumi na saba (17) ya supa jackpot katika bashiri ya supa jackpot.

5. Idadi ya juu ya bashiri pacha katika Supa Jackpot inaundwa na seti tofautitofauti za supa jackpot moja, elfu moja na ishirini na nne (1024) za tabiri 17 zilizowekwa katika bashiri moja ya supa Jackpot.

6.  Jumla ya gharama ya kiwango cha juu cha supa jackpot ya bashiri pacha itakuwa milioni moja na elfu ishirini na nne, kama ifuatavyo: (chaguzi za bashiri 1024*1,000 Sh. kwa kila bashiri = Sh. 1,024,000)

7.  Endapo utaweka pacha unganifu n, kila seti moja ya 2n ya tabiri 17 inachukuliwa kama bashiri binafsi na inaweza kushinda Supa Jackpot na/au bonasi (kama itatatolewa).

8. Endapo michezo mitatu au zaidi imefutwa, katishwa, achwa, sitishwa ama ahirishwa, Sportpesa yaweza, kwa kadri itakavyoona inafaa, ikafuta bashiri za Supa jackpot unganifu na kurudisha dau lililowekwa ndani ya masaa 72 ya kufutwa.

4.23.3.3. SUPA JACKPOT YA BASHIRI UNGANIFU PACHA TATU

1. Jiongezee faida zaidi na Supa jackpot ya bashiri pacha tatu kwa pamoja (bashiri unganifu pacha tatu) inayokuruhusu kufanya ubashiri kwa kufanya chaguzi tatu katika mchezo mmoja, kwa hadi michezo mitano kutoka katika orodha ya michezo kumi na saba ya supa jackpot katika bashiri moja ya supa jackpot.

2. Kadri unavyofanya bashiri pacha tatu kwa pamoja mara nyingi, ndivyo nafasi ya kushinda inavyoongezeka. Mahesabu ya idadi ya bashiri pacha tatu ni sawa na 3n (ambapo n ni idadi ya bashiri pacha tatu). Kwa mfano bashiri pacha tatu zikiwa tano (5) itakuwa sawa na 243(3*3*3*3*3) bashiri za supa jackpot moja.

3. Gharama ya bashiri unganifu pacha tatu inahesabiwa ifuatavyo: idadi ya miunganiko (3n, ambapo n ni idadi ya pacha tatu )* Sh. 1,000. Kwa mfano kwa bashiri pacha tatu zikiwa tano (5) za supa jackpot, gharama itahesabiwa kama 3*3*3*3*3=243 miunganiko *1,000/- = 243,000/- kwa bashiri iliyowekwa.

4. Bashiri unganifu pacha tatu yawezakuwa kwa kiwango cha chini chenye unganifu pacha tatu moja na hadi ukomo wa unganifu pacha tatu tano kutoka katika michezo kumi na saba (17) ya supa jackpot katika bashiri ya supa jackpot.

5. Idadi ya juu ya bashiri unganifu pacha tatu katika Supa Jackpot inaundwa na seti tofautitofauti za supa jackpot moja, mia mbili arobaini na tatu (243) za tabiri 17 zilizowekwa katika bashiri moja ya supa Jackpot.

6.  Jumla ya gharama ya kiwango cha juu cha supa jackpot ya bashiri unganifu pacha tatu itakuwa laki mbili na elfu arobaini na tatu, kama ifuatavyo: (chaguzi za bashiri 243*1,000 Sh. kwa kila bashiri = Sh. 243,000)

7.  Endapo utaweka bashiri pacha tatu unganifu n, kila seti moja ya 3n ya tabiri 17 inachukuliwa kama bashiri binafsi na inaweza kushinda VYOTE vifuatavyo:

(i) Supa Jackpot; 

(ii) Bonasi, kulingana na kwa kadri Sportpesa itavyoona inafaa.

8. Idadi ya juu ya bashiri unganifu pacha 5 na pacha tatu 5 katika Supa Jackpot inaundwa na seti tofautitofauti za supa jackpot moja, 7776(2*2*2*2*2*3*3*3*3*3) za tabiri 17 zilizowekwa katika bashiri moja ya supa Jackpot.

9. Unaweza kubashiri mkeka wa mechi 13 kati ya 17, mechi 14 kati ya 17, mechi 15 kati ya 17, mechi 16 kati ya 17 na mechi 17 ya 17.

4.24. KANUNI MAALUM KWAAJILI YA MICHEZO YA NGUMI/NDONDI

  1. 4.24.1. Kwa madhumuni ya kubashiri, pambano la ndodi /ngumi litachukuliwa kuwa limeanza pale kengele itakapopigwa kuashiria kuanza kwa mzunguko wa kwanza.
  2. 4.24.2. Matokeo ya mwishoni mwa mchezo wa ngumi ni ya mwisho. Hii ni pamoja na marudio ya hesabu za ‘kadi za alama’ za majaji.
  3. 4.24.3. Kwa madhumuni ya kubashiri, pambano la ndondi likitangazwa kuwa ‘sare ya kiufundi’ itapelekea matokeo ya sare kuchukuliwa kuwa ndio ushindi.
  4. 4.24.4. Mabadiliko yoyote yatakayofanywa baadae na vyombo husika hayatahesabika kwa madhumuni ya kubashiri.
  5. 4.24.5. Pale pambano la ndondi linapofanyika katika nchi tofauti na nchi iliyokusudiwa mwanzo, bashiri zote zitaendelea kuwa halali.
  6. 4.24.6 Endapo pambano la ndondi halitofanyika kwa sababu yoyote ile kwa tarehe iliyokusudiwa na halijafanyika ndani ya masaa 72 baada ya tarehe iliyokusudiwa mwanzo, basi bashiri zote zitakuwa batili.
  7. 4.24.7. Vigezo na Masharti vya Sportpesa vitatumika.
  8. 4.24.8. Ikiwa utatokea mgongano kati ya kanuni hizi maalum na Kanuni za SportPesa juu ya pambano la ndondi, kanuni hizi maalum zitatumika.

4.25. MPIRA WA KIKAPU

4.25.1. Michezo yote ni lazima ianze katika tarehe zilizopangwa (kwa majira yanayotumika katika dimba husika) ili bashiri zikubalike.

4.25.2. Endapo dimba lililopangwa mwanzo litabadilishwa, bashiri zilizofanywa zitaendelea ikiwa timu ya nyumbani itaendelea kuwa timu ya nyumbani. Ikiwa timu ya nyumbani na ya ugenini kwa mechi iliyo pangwa watacheza katika dimba la timu ya ugenini, bas bashiri zitakubalika ikiwa tu timu ya nyumbani itaendelea kuhesabika hivo rasmi, vinginevyo hizo bashiri zitabatilishwa.

4.25.3. Bashiri zote za kabla ya mechi zitahusisha muda wa nyongeza isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo.

4.26. TENISI

4.26.1. Kama kutatokea tukio lolote kati ya matukio yafuatayo, bashiri bado zitakubalika:

4.26.1.1. Mabadiliko ya ratiba na/au siku ya mechi

4.26.1.2. Mabadiliko ya uwanja

4.26.1.3. Mabadiliko kutoka kuchezea ndani ya ukumbi na kuchezea sehem ya wazi au kinyume chake

4.26.1.4. Mabadiliko ya sakafu “surface” (ama kabla au wakati wa mechi)

4.26.2. Ikiwa mechi itaanza na isimalizike basi ubashili wote uliofanywa utakuwa batili.

4.26.3. Kubashiri mechi za mashindano – wachezaji wanaopambanishwa katika mechi lazima wacheze pointi 1 katika mashindano ili ubashiri uhesabike. Endapo wachezaji wataendelea mbele kwenye raundi ile ile ya mashindano basi bashiri zitakuwa batili.

4.26.4. Kama kutatokea sare na itumike kuamua seti ya mwisho, hii itahesabiwa kama seti ndani ya mechi moja.

4.26.5. Bashiri kwa seti – ubashiri utakuwa batili endapo idadi ya seti kisheria hazitatimia, au zitabadilishwa.

4.26.6. Mshindi wa seti ya kwanza – endapo seti ya kwanza haitochezwa hadi mwisho, ubashiri utakuwa batili.

4.26.7. Handicap, Jumla ya Michezo katika Mechi na Michezo katika Masoko hutokana na mahitajio ya kisheria ya idadi ya seti (tazama kuhusiana na bashiri za seti).

4.26.8. Endapo idadi ya seti kisheria itabadilishwa au kutofautiana na zile zilizotolewa kwa madhumuni ya kubashiri basi bashiri zote zitakuwa batili.

4.27. MCHEZO WA RAGA

4.27.1. Isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo, bashiri zote za mchezo wa raga zitakamilishwa kwa kipindi cha dakika 80 za mchezo.

4.27.2. Isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo, ubashiri wa mechi za raga saba na kumi zinashughulikiwa kwa kuzingatia kanuni za mashindano husika na huweka kando muda wa ziada kama utakuwepo.

4.27.3. Endapo mechi itachezwa kwenye ukumbi tofauti na ule uliotangazwa basi ubashiri wote kwa mechi hiyo utakuwa batili

4.27.4. Endapo kutakuwa na mabadiliko ya mpinzani tofauti na yule aliyetangazwa basi ubashiri wote kwenye mechi hiyo utakuwa batili.

4.28. KRIKETI

4.28.1. Mechi zisizochezwa kama ilivyopangwa–Endapo uwanja wa mchezo utabadilishwa, bashiri zote zitakazokuwa zimefanyika zitahesabika ikiwa timu ya nyumbani itaendelea kuhesabiwa hivyo. Ikiwa timu ya nyumbani na ya ugenini katika mchezo uliopangwa zitabadilishwa, basi bashiri zitakazokuwa zimefanyika kwa kutumia orodha ya mwanzo zitakuwa batili.

4.29. MALIPO YA BASHIRI

4.29.1 Takwimu zitakazotolewa na watoaji rasmi wa matokeo ama tovuti rasmi ya mashindano husika au ratiba zitatumika katika kuamua malipo ya dau.

4.29.2. Kama takwimu kutoka kwa mtoaji rasmi au kwenye tovuti rasmi hazipatikani au kukiwa na ushahidi wa kutosha kuwa takwimu za mtoaji rasmi wa matokeo ama tovuti sio sahihi, tutatumia ushahidi huru kuamua malipo.

4.29.3. Kama hakuna ulinganifu, ushahidi huru ama kukiwa na ukinzani wa wazi katika ushahidi, bashiri zitalipwa kutumia takwimu zetu wenyewe.

4.30. JENGA BET

4.30.1 Kwa minajili ya Jengabets, taratibu zifuatazo zitatumika:

  • 4.30.1.1 Ikiwa chaguzi yako yoyote imebatilishwa, tutakurejeshea kiasi chote cha dau ulichoweka.
  • 4.30.1.2 Ikiwa mchezo utakatishwa, ahirishwa ama utaachwa, tutalipa ubashiri wowote utakaokuwa sahihi na kuchukulia kama úliopoteza' ubashiri wowote ambao hautokuwa sahihi wakati wa katisho, ahirisho ama kuachwa.

4.31. NAMBA ZA BAHATI

4.31.1. Bashiri zote za Namba za Bahati kwaajili ya droo maalum lazima zifanywe na kuthibitishwa kabla ya kuanza kwa droo, na kabla namba ya kwanza haijachezwa katika bashiri iliyofanywa.

4.31.2. Iwapo kwa sababu yoyote ile bashiri imefanywa baada ya namba ya kwanza kuchezwa, ubashiri utabatilishwa na kima kamili kilichochezwa kitarejeshwa.

4.31.3. Ikiwa muda wa droo utasogezwa mbele, droo itafutwa, na madau yote yatakayoathirika yatarejeshwa. Droo mpya yaweza fanyika kwa wakati utakaopangwa. 

4.31.4. Matokeo ya Droo za Namba za Bahati yatatokana na matokeo ya kwanza yaliyochapishwa katika tovuti rasmi za Numba za Bahati. Ikiwa kutakuwa na makosa yoyote na/ama matokea kubadilishwa na kuchapishwa mengine, droo itafutwa, na madau yote kurejeshwa.

4.31.5. Bashiri zote ambazo haziwezi kulipwa kwa sababu yoyote ile zitabatilishwa na dau husika kurejeshwa.

4.31.6. Masoko yote ya bashiri za Namba za Bahati ni ya oddi dhahiri (fixed odds), yenye matokeo ya aina moja, kupatia ama kukosa. Hakuna zawadi ya kifuta jasho (consolation prize) kwenye droo au soko lolote.Namba zote zilizochaguliwa lazima zioane na chaguzi ya bashiri katika mfuatano wowote au lazima zioane na soko lililo bashiriwa na lazima ziwe zimepatiwa sawasawa ili kushinda. 

4.31.7. Katika masoko ya bashiri ya kiwango, namba zote zilizochaguliwa kwaajili ya bashiri lazima zitokee kwa mfuatano sahihi ili kushinda.Kwa mfano, ikiwa zitachaguliwa namba nne (katika soko la namba 4) kwa oddi za 2275/1 na tatu kati ya zile namba nne zilizochaguliwa zimejitokeza, hakuna ushindi na hakuna malipo.

4.31.8. Ili ubashiri uwe sawa, mchezaji lazima achague aina ya soko, namba au matokeo anayotazamia kwenye droo, achague dau la kuweka na kufanya ubashiri kabla mpira wa kwanza wa droo ya Namba za bahati haujachaguliwa au muda wa mwisho wa kuanza haujaisha, ambapo baada ya hapo matokeo lazima yachapishwe sawasawa. Mara baada ya kuchapishwa kwa matokeo halali ya Namba za Bahati, malipo yote ya bashiri yatalipwa moja kwa moja kwenye akaunti ya mchezaji.

4.31.9. Ikiwa muda wa droo yoyote utaisha kabla ya ubashiri kukamilika, mchezajia anaweza kuhamishia madau haya kwenye droo nyingine itakayofuatia ama weweza kufutwa.

4.32. AINA ZA MASOKO NA MAELEZO YAKE

4.32.1. Jumla ya mipira iliyochaguliwa itakuwa witiri ama shufwa.
             Jumla ya mipira mfuatano itakayochaguliwa itakuwa witiri ama shufwa.

4.32.2. Jumla ya mipira itakayochaguliwa itakuwa juu ama chini
             Jumla ya mipira mfuatano itakayochaguliwa itakuwa juu au chini ya mpaka uliowekwa.

4.32.3. Jumla ya mipira mfuatano itakayochaguliwa itakuwa ndani ya wigo uliowekwa.
            Kuna aina tofauti tofauti kumi na nne za wigo ambao mchezaji aweza bashiri jumla ya ushindi. 

4.32.4. Mpira wa bonasi utakaochaguliwa utakuwa witiri ama shufwa.
             Mchezaji anabashiri iwapo mpira wa bonasi utakaochaguliwa utakuwa witiri au shufwa. Chaguo hili la bashiri ni kwaajili tu ya michezo yenye mpira mmoja wa bonasi.

4.32.5. Jumla ya mipira ya bonasi itakayochaguliwa itakuwa witiri ama shufwa.
             Mchezaji anabashiri iwapo jumla ya mipira ya bonasi itakayochaguliwa itakuwa witiri au shufwa.
             Chaguo hili la bashiri ni kwaajili tu ya michezo yenye mipira miwili ya bonasi. 

4.32.6. Mpira wa bonasi utakaochaguliwa utakuwa juu ama chini.
             Mchezaji anabashiri iwapo jumla ya mipira ya bonasi itakayochaguliwa itakuwa juu ama chini ya mpaka uliowekwa. Aina hii ya bashiri ni kwaajili tu ya michezo yenye mpira mmoja wa bonasi.

4.32.7. Jumla ya mipira ya bonasi itakayochaguliwa itakuwa juu ama chini.
             Mchezaji anabashiri iwapo jumla ya mipira ya bonasi itakayochaguliwa itakuwa juu au chini ya mpaka uliowekwa. Aina hii ya bashiri ni kwaajili tu ya michezo ya Namba za Baahati yenye mipira ya bonasi miwili.

4.32.8. Mpira wa bonasi utakaochaguliwa utakuwa ni wa namba ya tarakim moja.
             Mchezaji anabashiri iwapo mpira wa bonasi utakuwa ni wa namba moja ya tarakimu. Katika michezo ya Namba za Bahati yenye mipira miwili ya bonasi, walau mpira mmoja wa bonasi unapaswa uwe wa tarakim moja ili mchezaji ashinde. Soko hili                     halizihusu aina za droo zenye tarakim moja tu katika droo ya mpira wa bonasi. 

4.32.9. Mpira wa bonasi utakaochaguliwa utakuwa ni wa namba moja na moja ya mipira ya mfuatano itakayochaguliwa.
             Mchezaji anabashiri iwapo mpira wa bonasi utakuwa ni wa namba moja na moja ya mipira katika droo mfuatano. Ikitokea mipira ya bonasi miwili imechaguliwa kutoka kwenye kapu la nyongeza, mchezaji atakuwa ameshinda ikiwa mojawapo ya                         mipira ya bonasi itakayochaguliwa ni sawa na mpira wowote uliochaguliwa kwenye droo mfuatano.

4.32.10. Jumla ya mipira ya bonasi itakayochaguliwa itakuwa ndani ya wigo uliowekwa.
               Mchezaji anabashiri iwapo mpira wa bonasi uliochaguliwa utakuwa ndani ya moja ya wigo 5 zilizotolewa. Chaguo hili la bashiri ni kwaajili tu ya michezo ya Namba za bahati yenye mpira wa bonasi mmoja.

4.32.11. Jumla ya mipira mfuatano na mipira ya bonasi itakuwa juu ama chini.
               Mchezaji anabashiri iwapo jumla ya namba zzilizochaguliwa ikiwemo mpira wa bonasi itakuwa juu au chini ya mpaka uliowekwa.

4.32.12. Bashiri ya kiwango (bila mpira wa bonasi).
               Kutegemeana na aina ya mchezo wa Namba za Bahati, wachezaji wanachagua namba ambazo wanaamini zitachaguliwa; ili kushinda zawadi, mchezaji lazima abashiri namba zote zilizochaguliwa. Namba zote zilizochaguliwa kwenye bashiri moja                         lazima zitokee ili bashiri iwe ya ushindi.

4.32.12. Bashiri ya kiwango (bila mpira wa bonasi).
               Kutegemeana na aina ya mchezo wa Namba za Bahati, wachezaji wanachagua namba ambazo wanaamini zitachaguliwa; ili kushinda zawadi, mchezaji lazima abashiri namba zote zilizochaguliwa. Namba zote zilizochaguliwa kwenye bashiri moja                         lazima zitokee ili bashiri iwe ya ushindi.

4.32.13. Bashiri ya kiwango (ikiwa ni pamoja na mpira wa bonasi kutoka kwenye kapu la nyongeza) 
               Wachezaji wanachagua namba kulingana na kanuni za bashiri ya kiwango, lakini mizania ya ushindi inaongezeka kadri matokeo ya mpira wa bonasi yanavo hesabika pia.Namba zote zilizochaguliwa katika bashiri moja lazima zitokee ili kushinda. 

4.32.14. Bashiri ya kiwango (ikiwemo mpira wa bonasi kutoka kwenye kapu la nyongeza).
               Wachezaji wanachagua namba kulingana na kanuni za bashiri ya kiwango, lakini mizania ya ushindi inaongezeka kadri ushindi wa mpira wa bonasi unavyohesabika pia. Ikiwa mipira miwili ya bonasi itatokea, mchezaji lazima aoanishe namba zilizochaguliwa kutoka kwenye droo ya mfuatano, na moja ya mipira ya bonasi ili aweze kushinda. Namba zote zilizochaguliwa katika bashiri moja lazima zichaguliwe ili iweze kuwa bashiri ya ushindi. 

4.33. ASIAN HANDICAP

4.33.1. Asian Handicap +0.75/-0.75 inamaanisha – Bashiri kuanza ikiwa na faida juu ya goli (+0.75) ama kuanza ikiwa na pungufu kwenye goli (-0.75). Ikiwa umechagua +0.75 bashiri yako itashinda ikiwa timu uliyochagua itashinda ama kutoa sare. Ikiwa timu yako itapoteza kwa tofauti ya goli moja, utarudishiwa nusu ya dau uliloweka na kupoteza nusu nyingine.Kwa kifupi, matokeo yawezakuwa Kushinda, Kushinda nusu, Kupoteza nusu au Kupoteza kabisa.  

4.33.2. Asian Handicap +1.25/-1.25 inamaanisha – Bashiri kuanza ikiwa na faida juu ya goli (+1.25) ama kuanza ikiwa na pungufu kwenye goli (-1.25). Ikiwa umechagua +1.25 bashiri yako itashinda ikiwa timu uliyochagua itashinda ama kutoa sare. Ikiwa timu yako itapoteza kwa tofauti ya goli moja, utarudishiwa nusu ya dau uliloweka na kushinda nusu nyingine. Kwa kifupi, matokeo yawezakuwa Kushinda, Kushinda nusu, Kupoteza nusu au Kupoteza kabisa.

4.33.3. Asian Handicap Over/Under 0.75  - Hii inamaanisha, kwa bashiri ya 0.75, utapaswa kugawa dau lako katika bashiri mbili: Nusu ya dau lako linawekwa kwenye handicap ya 0.5 na nusu nyingine kwenye handicap ya goli 1. Ikiwa magoli mawili au zaidi yatafungwa, bashiri ya Over 0.75 imeshinda jumla wakati ile ya Under 0.75 haitokupa kiwango chochote cha pesa. Kwa kifupi, matokeo yawezakuwa Kushinda, Kushinda nusu, Kupoteza nusu au Kupoteza kabisa.  

4.33.4. Asian Handicap Over/Under 1.25 - Hii inamaanisha, kwa bashiri ya 1.25, utapaswa kugawa dau lako katika bashiri mbili: Nusu ya dau lako linawekwa kwenye handicap ya 1.00 na nusu nyingine haandicap ya goli 1.50. Ikiwa magoli mawili au zaidi yatafungwa, bashiri ya Over 1.25 imeshinda jumla wakati ile ya Under 1.25 haitokupa kiwango chochote cha pesa. Kwa kifupi, matokeo yawezakuwa Kushinda, Kushinda nusu, Kupoteza nusu au Kupoteza kabisa. 

4.34 CASH OUT

4.34.1. Huduma hii inakuruhusu kupata malipo ya mapema katika bashiri zako kabla ubashiri wako na matokeo hayajamalizika, pia Cashout itatumika kwa multibet ya mchezo wa mpira pekee.

4.34.2. Cash out inapatikana kwenye odds za mechi ambazo hazijaanza kuchezwa. 

4.34.2. Cash out inapatikana kwenye odds za mechi ambazo hazijaanza kuchezwa. 

4.34.4. Cash Out haiwezekani endapo:

  • 4.34.4.1. Kwenye bashiri, zilizo na chaguzi za kukosa.
  • 4.34.4.2. Ikitokea hakuna odds kwa ajili ya chaguzi za bashiri.
  • 4.34.4.3. Kwenye bashiri moja.

4.34.5. Baada ya kutoa pesa, bashiri yako itahesabika imeshalipwa, bila kujali matokeo ya mchezo.

4.34.6. Kuangalia na Kujaribu machaguo yaliyopo, tafadhali angalia historia katika kurasa yako ya kubeti.

4.34.7. Kampuni italipa kwa wakati ila haitawajibika kwenye ulipaji wa mapema au kuchelewa ambao unaweza kuathiri kikomo cha malipo yasiku ya mteja.

5. MALALAMIKO, MIGOGORO, SHERIA TAWALA NA MAMLAKA ZA UAMUZI
+

5.1 Endapo kutakuwa na madai yoyote au mgogoro utokanao na muamala wa zamani au wa sasa, tafadhali wasiliana nasi. Ikiwa Kampuni itashindwa kutatua mgogoro, Kampuni itawasilisha mgogoro huo kwa msuluhishi, kama Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ambapo uamuzi wao utakuwa wa mwisho (isipokuwa kukiwa na makossa ya wazi) na wahusika wote watawakilishwa ipasavyo. Hakuna mgogoro utokanao na bashiri/dau utakaopelekea magomvi ya mahakamani, shitaka la kimahakama ama pingamizi juu ya leseni au kibali cha mwendesha bashiri (ikiwemo leseni ya mwendeshaji mwingine au ya Kampuni) isipokuwa kama Kampuni itashindwa kutekeleza uamuzi uliotolewa na msuluhishi ama Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ambapo waweza fikisha suala lako katika mahakama yenye malaka juu ya suala hilo.

5.2 Malipo ya ubashiri kwa michezo ya Tanzania: Daima ubashiri kwa michezo ya Tanzania utalipwa kulingana na takwimu na matokeo yatolewayo na chombo kinachosimamia mchezo husika mf. Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) (ukiondoa makosa ya wazi).

5.3 Kanuni hizi na pia mgogoro au madai yoyote yatokanayo na au yahusianayo na Kanuni hizi au jambo linalobishaniwa, vitatawaliwa na kutafsiriwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania bila kujali mchezaji anatokea wapi.

5.4 Kwa kukubalina na Kanuni hizi na/au kufanya ubashiri ama kuweka dau na/au kutumia (ikiwa umeruhusiwa au la) vifaa ama huduma zitolewazo na Kampuni (aidha kwa kutumia huduma ya simu, tovuti pamoja na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, ama vinginevyo) unakubalia kwa kwamba mahakama za Tanzania zitakuwa na mamlaka pekee ya kutatua mgogoro wowote unaoweza kutokea kutokana na au kuhusiana na Kanuni hizi. Bila kujali yaliyotamkwa hapo juu, Kampuni itakuwa na haki ya kufikisha madai dhidi ya mteja katika mahakama ya nchi anakoishi.

6. OFA, BONASI NA PROMOSHENI
+

6.1. Ofa zote kwa wateja zitakuwa na ukomo wa ofa moja kwa kila namba ya simu iliyosajiliwa. Tutakuwa na haki ya kuondoa/kusitisha ofa yoyote ama ofa zote kwa mteja yoyote wakati wowote na kwa matakwa yetu pekee bila kuingiliwa ama kushinikizwa na mtu.

6.2. Endapo kipengele chochote cha ofa ama promosheni kitakiukwa au kukiwa na ushahidi wowote juu ya mlolongo wa bashiri/ madau yalowekwa na mteja ambayo kutokana na bonasi alizopata zinamwezesha kufanya malipo wezeshi, kubashiri bure ama ofa yoyote ya promosheni inayompelekea mteja kuwa na uhakika wa faida bila kujali matokeo, aidha akiwa mwenyewe ama sehemu ya kundi, Kampuni itakuwa na haki ya kuondoa bonasi kutoka kwenye ofa husika na kwa maamuzi ya Kampuni pekee, kulipa bashiri kwa odds sahihi, kubatilisha bashiri–bure au kubatilisha bashiri/dau lolote lililowezeshwa kwa pesa ya bonasi. Na pia, Kampuni itakuwa na haki ya kutoza ushuru wa gharama za usimamizi kwa mteja kwa kiasi cha amana ya bonasi, bashiri/dau–bure au malipo ya ziada ili kufidia gharama za usimamizi. Kampuni pia itakuwa na haki ya kumtaka kila mteja kutoa nyaraka za kutosha ili Kampuni ijiridhishe kwa kadri ionavyo inafaa, na utambulisho wa mteja kabla Kampuni haijaweka bonasi yoyote, bashiri ya bure au ofa kwenye akaunti ya mteja.

6.3. Kampuni ina haki ya kurekebisha vigezo vya au kufuta ofa yoyote wakati wowote.

6.4. PROMOSHENI YA RAFIKI BONASI

6.4.1. Sasa ni rahisi kusaidia marafiki zako kujiunga na mchezo huu kupitiapromosheni ya Rafiki Bonasi.

6.4.2. Promosheni ya Rafiki bonsai ilianza saa 6.01 usiku, Jumatatu ya tarehe 7 Agosti 2017.

 6.4.3. Rafiki bonasi iko wazi kwa washiriki wa Sportpesa wa zamani na wapya. Unahitaji tu kumwalika rafiki, kumjulisha aandike namba yako ya simu kama namba iliyomkaribisha na kisha kumwacha aweke bashiri yake. Kwa kila rafiki aliekaribishwa, mteja aliemkaribisha atakuwa na haki ya kupata bonasi ya Sh. 2000.00 ikiwa mteja aliekaribishwa ataweka dau la Sh. 2000.00 au zaidi. Ikiwa mteja aliekaribishwa ataweka dau lolote lililochini ya Sh. 2000.00, mteja aliemkaribisha atakuwa na haki ya kupata kiasi kinacholingana na dau lililowekwa. Kwa minaajili ya Rafiki bonasi, kiasi kinachohesabika ni kile cha ubashiri wa mwanzo tu.

6.5 PROMOSHENI YA JACKPOT

6.5.1 Kampuni yaweza, mara kwa mara, kufanya promosheni ya jackpot. Utaarifiwa kupitia tovuti yetu, mitandao ya kijamii ama njia nyingine yoyote kila mara promosheni hiyo itakapokuwa ikifanyika.Utaratibu na Masharti yafuatayo yatatumika kwa kila promosheni ya jackpot isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo.

6.6. Promosheni ya Betspinner

6.6.1. Unapo shiriki kwenye promosheni hii, unaweza kujishindia bonasi kwa kuzidisha juu ya kiasi ulichotakiwa kushinda awali.

6.6.2. Utakapo shiriki promosheni hii uaweza kujishindia bonasi ya mpaka asilimia mia moja juu ya kiwango ulicho takiwa kushinda awali.

6.7. Promosheni ya Goal Rush.

6.7.1. Promosheni ya Goal Rush ni promosheni ya kila siku ambayo ni bure kucheza na inampa Mteja haki ya kupata ingizo moja tu kwa kila awamu ya promosheni.

6.7.2. Ili kushiriki katika promosheni hii, mteja lazima:

6.7.2.1. amefanikiwa kusajili akaunti na Kampuni.

6.7.2.2. Ingia na kuweka ubashiri wake kwa kutumia akaunti yake.

6.7.2.3. ameweka dau la kulipia kwenye app ya Kampuni katika siku 7 zilizopita.

6.7.2.4. Shiriki ubashiri wake kwenye jukwaa la mitandao ya kijamii kama inavyoamuliwa na Kampuni kwa hiari yake.

6.7.3. Unashiriki promosheni hii kwa kuchagua, katika kila mechi kutoka kwa ratiba iliyopendekezwa, timu ambayo itafunga bao la kwanza na dakika mahususi ambayo bao hilo litafungwa. Kiingilio kwa kila raundi kinapatikana baada ya kushiriki ubashiri wako kwenye jukwaa la mitandao ya kijamii linaloruhusiwa na kabla ya mechi ya kwanza kuanza. Huwezi kurekebisha ingizo lako mara tu litakapowasilishwa.

6.7.4. Ratiba zilizopendekezwa zilizojumuishwa katika kila awamu ya promosheni ya Goal Rush huamuliwa na Kampuni pekee.

6.7.5. Ikiwa ingizo lako litatabiri kwa usahihi wakati bao la kwanza litakapofungwa katika mechi zote tatu zilizopendekezwa zilizojumuishwa katika kila raundi ya Goal Rush, mteja atashinda Zawadi.

6.7.6. Unaposhiriki katika promosheni ya Goal Rush, utazawadiwa zawadi ya jumla ya hadi TZS Milioni Mia Moja (100,000,000/-) juu ya malipo ya juu zaidi, zawadi ya juu ya kila siku ya TZS 200,000/= na hamsini wanaofuata zawadi ya TZS. 10,000/= kila utabiri wako ukishinda.

6.7.7. Pale ambapo kuna washindi wengi wa Zawadi katika awamu yoyote ya promosheni  ya Goal Rush, kiasi cha Zawadi kitagawanywa kwa usawa miongoni mwa washindi wote wa Zawadi.

6.7.8. Pale ambapo mechi imeahirishwa au kukosekana kwa suluhu ya kawaida, mchezo huo hautahesabiwa tena kuelekea Goal Rush. Muundo wa zawadi kwa raundi hiyo utarekebishwa kulingana na idadi ya mechi zilizosalia na kuonyeshwa katika sehemu ya Goal Rush. Ratiba mbili au zaidi zikiahirishwa au zikibatilika, raundi nzima ya Goal Rush itatatuliwa kama batili.

6.7.9. Zawadi kwa kila awamu ya Matangazo ya Goal Rush zitatolewa mara tu matokeo ya mechi husika yatakapojulikana.

6.7.10. Akaunti yako inaweza kuwa chini ya ukaguzi wa kawaida wa uthibitishaji kabla ya kuondolewa kwa ushindi kwenye Matangazo ya Goal Rush.

6.7.11. Promosheni ya Goal Rush inapatikana kwa uamuzi wa Kampuni na Kampuni haitoi hakikisho kuhusu upatikanaji wake. Kampuni haitawajibika ikiwa Ukuzaji wa Goal Rush haupatikani kwa sababu za kiufundi.

6.7.12. Kampuni inahaki ya kukubali au kukataa ingizo lolote la Goal Rush.

6.7.13. Kampuni inahaki ya kurekebisha, kusimamisha au kuondoa Matangazo ya Goal Rush (au sehemu yake yoyote) kwa tukio lolote, muundo au mteja.

6.7.14. Kampuni inahaki ya kuondoa Matangazo ya Goal Rush kwa mteja au kikundi chochote cha wateja ambapo ina misingi ya kuridhisha ya kuamini kuwa mteja au vikundi vya wateja vinatumia Promosheni hii vibaya.

6.7.15. Kila mshiriki anastahili kushinda zawadi moja tu kwa siku.

6.7.16. Timu yetu ya huduma kwa wateja itampigia simu mshindi mara tatu ili kuthibitisha utambulisho wao na kumtaarifu kuhusu ushindi wake.

6.7.17. Ikiwa mshindi hatopokea simu hizi, ushindi wake utafutwa, na zawadi itatolewa kwa mshiriki mwingine atakayepokea simu.

6.7.18.  Baada ya kushiriki, chapisho linapaswa kubaki kwenye ukurasa wa kijamii kwa muda usiopungua siku thelathini.

6.7.19. Iwapo mechi moja itaahirishwa, kuingiliwa, kuachwa au kusimamishwa kabla ya goli la kwanza kufungwa na mechi zote mbili hazitachezwa hadi kuhitimishwa ndani ya saa ishirini na nne (24)  baada ya hapo, mzunguko mzima wa promosheni hiyo maalum ya Goal Rush itakuwa  imebatilishwa. Kwa ufafanuzi zaidi, hakuna zawadi itakayotolewa katika raundi hii.

6.7.20. Iwapo zaidi ya mechi moja itaahirishwa, kuingiliwa, kuachwa, au kusimamishwa kabla ya bao ya kwanza kufungwa na mechi zote mbili hazitachezwa hadi kuhitimishwa ndani ya saa Ishirini na Nne (saa 24) baada ya hapo, mzunguko mzima wa promosheni hiyo maalum ya Goal Rush itakuwa. imeghairiwa. Kwa kuepusha shaka hakuna Tuzu zitakazotolewa katika hali hii.

7. FARAGHA

7.1. Dhumuni la sera hii ni kukufahamisha namna gani tutatumia taarifa zako zozote binafsi unazotoa kupitia huduma hii / jukwaa au huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/ majukwa ya kielektroniki. Tafadhali isome kwa makini kabla ya kutupatia taarifa yako yoyote binafsi.

7.2. Tunakusanya taarifa binafsi zifuatazo kutoka kwako ili uweze kujisajili na kutumia huduma hii/jukwaa au huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, na Michezo yetu, taarifa hizo ni pamoja na; jina lako, tarehe ya kuzaliwa, nyaraka za utambulisho na taarifa zako za mawasiliano ikiwa ni pamoja na namba ya simu na barua pepe.

7.3. Tunatumia taarifa zako za mawasiliano kukutumia jumbe zetu mara kwa mara kuhusiana na michezo mbalimbali pamoja na promosheni. Utaweza kujitoa katika hatua yoyote kwa kutuma ujumbe mfupi “toa” au “simamisha” kwenda kwenye namba ya Kampuni 15888. Iwapo utaendelea kupokea jumbe zetu hata baada ya kutuma ujume wa kujitoa, tafadhali wasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja mara moja.

7.4. Kampuni haitotoa taarifa zako binafsi kwa mtu mwingine yeyote, isipokuwa kama kutoa huko:

7.4.1 ni kwa mijubu wa sheria ambayo tuna wajibu wa kuitii, au kwaajili ya kutekeleza ama kutii Kanuni zetu na mikataba mingine ama kwaajili ta kulinda haki au mali zetu.

7.4.2. kunahitajika kwa madhumuni ya kufanya masoko ambapo umekubali bayana wakati wa usajili kuwa ungependa kupokea taarifa kutoka kwa mtandao wa washirika wetu, watoa matangazo na washirika wetu kuhusiana na bidhaa na huduma zao.

7.5. Pia tunaweza kutumia huduma za mtu mwingine huru ili kutusaidia kutoa huduma zetu mtandaoni. Wakati mwingine, watu hawa wanaweza kupokea taarifa zako. Hata hivyo, wakati wote, tutadhibiti na kuwajibika kwa matumizi ya taarifa zako.

7.6. Una haki ya kuona taarifa za miamala na historia ya ubashiri uliofanya nasi baada ya uthibitisho kwenye tovuti yetu.

7.7. Wewe ndiwe mtu pekee ulieruhusiwa kupitia, kusahihisha, kuongeza au kubadilisha taarifa zako binafsi wakati wowote.

7.8. Tumeweka mikakati ya makusudi ya kiufundi na ya kitaasisi yenye lengo la kulinda usalama wa taarifa zako dhidi ya upotevu wa bahati mbaya au kufikiwa, kutumiwa ama kubadilishwa au kuvujishwa na watu wasioruhusiwa. Hata hivyo, mtandao ni mfumo wa wazi na hatuwezi kuhakikisha kuwa watu wasio na ruhusa hawatoweza kuishinda mipango hiyo ya usalama au kutumia taarifa zako binafsi kwa madhumuni yasiyofaa. Pia, hatuwezi kuhakikisha kuwa mawasiliano yoyoyte, ujumbe au kiambatanishwa chochote hakitokuwa na virusi, hakitokuwa na namba zenye dhumuni la kukudhuru au haiendani na mfumo wako wa kielektroniki na hatukubali dhamana kuhusiana na virusi, namba zenye dhumuni la kudhuru au tatizo lolote linalohusiana ambalo linaweza kukupata.

7.9. Endapo tutafanya mabadiriko katika hizi sera zetu kwa njia yoyote ile, tutaweka toleo jipya lenye hayo mabadiriko kwenye tovuti yetu ya www.sportpesa.co.tz. Kutembelea tovuti hii mara kwa mara kunahakikisha kuwa daima unaelewa taarifa tunazokusanya, tunavyozitumia na katika mazingira gani, kama yapo, tutaweza kuzitoa kwa watu wengine.

7.10. Mazingira kama yalivyoainishwa katika sheria husika inayo simamia shughuli za Kampuni yanaweza kututaka kutoa taarifa zako kwa Mamlaka husika.

7.11. Kampuni haitowajibika kwa hasara yoyote au madhara yanayoweza kutokea kutokana na watu wasioruhusiwa kupata taarifa zako.

8. MATUMIZI YA HUDUMA, TOVUTI NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI/MAJUKWAA YA KIELEKTRONIKI
+

8.1. Taarifa pamoja na maudhui ya taarifa utakazozipata kwenye huduma ya simu, tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki (ikiwemo matokeo, takwimu, taarifa za michezo na orodha ya ratiba, odds na takwimu za kubashiri) ni kwaajili ya matumizi yako pekee na ni marufuku kuzisambaza ama kuzitumia kwa shughuli yoyote ya kibiashara. Hata hivyo, hakuna dhamana inayotolewa juu ya upatikanaji wa uhakika, usahihi ama matokeo yatokanayo na matumizi ya taarifa hizo. Taarifa hiyo haikusudii kuwa ushauri au mapendekezo na inatolewa kwaajili ya kukuhabarisha tu. Haipaswi kutumiwa kama kigezo cha kufanya ubashiri/kuweka dau, ambavyo vinafanywa kwa dhamana na hiari yako pekee.

8.2. Kompyuta yako au sim yako ya kiganjani na huduma ya mtandao vyaweza kuathiri utendaji na/au uendeshaji wa huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki. Kampuni haichukui dhamana kwamba huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, vitafanya kazi bila hitilafu au makosa au kwamba huduma za Kampuni zitatolewa bila kukatishwa. Kampuni haitowajibika kwa lolote kwa kushindwa au changamoto zinazotokana na matumizi ya kifaa chako, kuunganishwa kwa mtandao, mtandao au mtoa huduma za simu (ikiwemo kwa mfano, kushindwa kufanya ubashiri ama kuweka dau au kutazama au kupokea taarifa Fulani kuhusiana na matukio Fulani).

8.3. MATUMIZI YA HAKI

8.3.1 Huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki na bidhaa za Kampuni vinaweza kutumika kwa madhumuni ya kufanya ubashiri kwenye matukio na/au bidhaa tu.

8.3.2 Hutakiwi kutumia huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki kwa madhumuni ambayo (kwa maoni ya Kampuni) ni kinyume cha sheria, kashfa, matusi au machafu au ambayo kampuni inayaona kuwa ya kibaguzi, udanganyifu, uwongo au yasiyofaa.

8.3.3 Kampuni itachukua hatua za kijinai na za kimkataba dhidi ya mteja yeyote atakaejihusisha na vitendo vya ulaghai, kukosa uaminifu au vitendo vya jinai kupitia ama kuhusiana na huduma ya Simu, Tovuti, na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki au bidhaa za Kampuni. Kampuni itazuia malipo kwa mteja yeyote endapo lolote kati ya haya litashukiwa. Mteja atairudishia na atawajibika kikamilifu kuilipa Kampuni, itakapo dai, Madai yote (kama ilivyofafanuliwa hapo juu) yanayotokana moja kwa moja au vinginevyo, na kitendo cha mteja kudanganya, kukosa uaminifu ama cha jinai.

8.4 MASUALA YA PROGRAMU NA TEKNOLOJIA

8.4.1 Unaruhusiwa tu kutumia programu yoyote na programu nyingine zote zinazopatikana kwako kupitia huduma ya Simu, Tovuti, au vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, kwa madhumuni ya kutumia bidhaa zetu katika kifaa chako cha Simu au vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, na isipokuwa pale tu inaporuhusiwa na sheria husika, si kwa madhumuni mengine yoyote.

8.4.2 Tunakupatia haki binafsi, isiyo ya kipekee na isiyo hamishika, kutumia programu husika, kwa dhumuni pekee la kutumia /kucheza bidhaa kwenye vifaa vya simu na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, kwa mujibu wa vipengele vifuatavyo:

  • 8.4.2.1.: HURUHUSIWI KU:
    • 8.4.2.1.1. hamishia au pakia programu kwenye seva au vifaa vyenye mtandao au kuchukua hatua nyingine kufanya programu ipatikane kupitia mfumo wowote wa “bulletin board”, huduma ya mtandao au mfumo mwingine wowote wa huduma za mtandao kwa mtu mwingine yeyote;
    • 8.4.2.1.2. toa leseni ndogo, toa, kodisha, pangisha, kopesha, hamisha au nakili (isipokuwa kama kanuni hizi zimeeleza vinginevyo mahala popote) leseni yako kutumia programu au kufanya au kusambaza nakala za programu.
    • 8.4.2.1.3. ingia, pata au jaribu kuingia au kupata au vinginevyo kupenya mfumo wa usalama wa Kampuni au kuingilia kwa namna yoyote (pamoja na, lakini sio tu: roboti au viifaa vingine vya aina hiyo) kwa bidhaa husika au huduma ya Simu, na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, mabadiliko yoyote kwenye programu na/au visifa vyake au vitu vinavyoiunda;
    • 8.4.2.1.4. nakili au tafsiri nyaraka yoyote ya mtumiaji iliyotolewa ‘mtandaoni’ au katika mfumo wa kielektroniki.
  • 8.4.2.2. Na pia, isipokuwa kwa kiwango ch chini kilichoruhusiwa na sheria husika kuhusiana na programu za kompyuta, (ikiwemo madhumuni yaliyoruhusiwa kwa mujibu wa Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2015 ya Sheria za Tanzania au sheria yoyote inayoibadilisha/kufuta na/au kurekebisha sheria tajwa na sheria nyingine yoyote inayohusika) huruhusiwi ku:
    • 8.4.2.2.1. tafsiri, badli uhandisi, tawanya, achanisha, rekebisha, tengeneza kazi ambatani kwa kuiga, au kugeuza programu; au
    • 8.4.2.2.2. badili uhandisi, tawanya, achanisha, rekebishai, iga, tafsiri, fanya jaribio lolote kugundua namba ya siri ya chanzo cha programu au kutengeneza kazi ambatani kwa msingi wa programu yote au sehemu yake yoyote.

8.4.3. Haumiliki programu hii. Programu hii inamilikiwa na ni mali Kampuni pekeake au mtoa huduma ya programu mwingine (Mtoa Huduma wa Programu). Programu yoyote na nyaraka zinazoambatana nayo ambazo Kampuni imepewa leseni ya kuzitumia, ni bidhaa zinazomilikiwa na Mtoa huduma wa Programu na zinalindwa dunia nzima na sheria ya hati miliki. Utumiaji wako wa programu haukupi umiliki wa haki miliki yoyote kwenye programu hii.

8.4.4. Programu imetolewa ‘kama ilivyo’ bila ahadi zozote, masharti, dhamana au kauli zozote, aidha bayana au kwa taadhira, za kisheria ama vinginevyo. Kampuni inajitenga na vigezo vyote vya taadhira, masharti na ahadi (ikiwemo juu ya uuzikanaji, ubora wa kuridhisha na uimara kwa dhumuni lolote maalum). Kampuni haitoi ahadi yoyote kwamba:

  • 8.4.4.1. programu itatimiza mahitaji yako;
  • 8.4.4.2. programu haitokiuka haki miliki ya watu wengine
  • 8.4.4.3. utendaji wa programu hautokuwa na makosa au kuingiliwa
  • 8.4.4.4. Kasoro zozote kwenye programu zitasahihishwa, au
  • 8.4.4.5. Programu au vihifadhi taarifa hazitokuwa na virusi.

8.4.5. Endapo kutakuwa na makosa ya kimawasiliano au kimfumo kuhusiana na mahesabu ya kifedha au sehemu za programu, si Kampuni wala Mtoa Huduma wa Programu atawajibika kivyovyote vile kwako au kwa mtu mwingine yeyote, kuhusiana na makosa hayo. Kampuni itakuwa na haki, endapo makosa kama hayo yatatokea, kuondoa bidhaa zote husika kutoka kwenye huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, na kuchukua hatua nyingine yoyote kurekebisha makosa hayo.

8.4.6. Unakiri kuwa namna utakavyotumia programu, Kampuni haina uwezo wa kukusimamia. Hivyo basi, unapakua na kutumia programu kwa dhamana yako mwenyewe. Kampuni haitowajibika kwa lolote kwako au mtu mwingine yeyote kuhusiana na kupokea kwako kwa /au kutumia programu.

8.4.7. Programu yawezakuwa na taarifa za siri ambazo ni nyeti na zenye thamani kwa mtoa Huduma wa Programu na/au Kampuni. Huna haki ya kutumia au kufichua taarifa hizo za siri isipokuwa tu kwa mujibu Kanuni hizi.

8.4.8. Wakati Kampuni inajitahidi kuhakikisha kuwa huduma za Simu, Tovuti na vyombo vingine vya mawasiliano/majukwaa ya kielektroniki zinapatikana kwa saa 24 za siku, Kampuni haitowajibika iwapo kwa sababu yoyote huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya mawasiliano/majukwaa ya kielektroniki hayapatikani muda wowote au kwa kipindi chochote. Tutakuwa na haki ya kufanya mabadiliko au marekebisho kwa au kubadili, kuahirisha au kusitisha sehemu yoyote ya maudhui au huduma au bidhaa zilizopo, pamoja na uwezo wako wa kupata huduma hiyo.

8.4.9. Hupaswi kutumia vibaya huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielectroniki kwa kuingiza virusi, Trojan, minyoo, mantiki bomu au vitu vingine ambavyo ni haribifu au vina madhara kiteknolojia. Na haswa, hupaswi kupata bila ruhusa, kuingilia kati, kudhuru au kuvuruga huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya mawasiliano/majukwaa ya kielektroniki, au sehemu yake yoyote; kifaa chochote au mtandao ambapo taarifa zinahifadhiwa; na programu yoyote inayotumika kuhusiana na utoaji wa huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki; au kifaa chochote, programu inayomilikiwa au kutumiwa na mtu mwingine. Hupaswi kushambulia huduma zetu za simu, tovuti na vyombo vingine vya habari/ majukwaa ya kielektroniki, kupitia shambulizi la kunyimwa-kwa-huduma. Hatutahusika kwa hasara yoyote au madhara unayosababishwa na kusambazwa kwa mashambulizi ya kunyimwa-kwa-huduma, virusi au vitu vingine vyenye madhara kiteknolojia vyenye uwezo wa kuambukiza kifaa chako cha komputa, programu za kompyuta, taarifa au vifaa miliki vingine kutokana na matumizi yako ya programu au kwa kupakua kitu chochote kilichotumwa kwenye programu yako, au kwenye huduma yoyote ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, vilivyounganishwa.

9. MAUDHUI YA MTU WA TATU
+

9.1. Kampuni inapokea taarifa mrejesho, fafanuzi na maudhui kutoka kwa watoa huduma mbali mbali. Baadhi ya watoa huduma wanaweza kuhitaji ukubaliane na vigezo na masharti ya ziada yanayosimamia utumiaji wa taarifa, matangazo na maudhui. Kama hautokubaliana na vigezo na masharti ya mtu husika, usitumie taarifa, matangazo wala maudhui yake.

9.2. Kampuni haitowajibika kwa namna yoyote ile kuhusiana na taarifa, matangazo, na maudhui ya mtu wa tatu.

9.3. Kampuni hairuhusu mwajiriwa yoyote, mtu mwingine yeyote yule anayehusiana na mwajiriwa au mtu mwingine anayehusiana na mtoa huduma mwingine (kama itakavyoamriwa na Kampuni kwa kadri itakavyoona inafaa) kubashiri kwenye soko lolote au tukio lolote ambapo mtoa huduma wa tatu anatoa huduma kwa Kampuni. Kampuni itabatilisha ubashiri wowote itakapoona kwa hiari yake yenyewe kuwa ubashiri huo umetendeka.

9.4. Endapo Huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, vina nyenzo ya kuunganishwa na rasilimali za mtu wa tatu, nyenzo hizo zimewekwa kwa kukutaarifu tu. Kampuni haina uwezo wa kuingilia maudhui ya nyanja hizo au rasilimali na haitowajibika kwa lolote kwaajili yake au kwa hasara au madhara yanayoweza kutokea kutokana na wewe kutumia rasilimali hizo. Kuwekwa kwa nyenzo kukufikisha kwa mtu wa tatu hakumaanishi kukubaliana na huduma wala bidhaa zake (kama zinatumika).

10. UWAJIBIKAJI
+

10.1 Kampuni haitowajibika kutokana na makosa yoyote kuhusiana na bashiri au dau ikiwa ni pamoja na pale ambapo:

  • 10.1.1. Kampuni imekosea kuandika jumla ya odds/spreads/handicap husika;
  • 10.1.2. Kampuni inaendelea kupokea bashiri/dau kwenye masoko yaliyofungwa au kusitishwa;
  • 10.1.3. Kampuni imekosea kuhesabu au kulipa kiasi cha malipo; au
  • 10.1.4 makosa yoyote yanayotokea kwenye kifaa cha kuamua matokeo (Random Number Generator–RNG) au meza za malipo zilizoambatanishwa au kutumika kwenye mchezo wowote au bidhaa.

10.2. Bei isiyo Sahihi – Kabla ya tukio kuanza, wakati wa mchezo/kucheza au baada ya tukio, endapo kosa la wazi litagundulika, bashiri zozote za wazi zitakubalika na zitalipwa kwa kiasi kipya kilichowekwa upya na Kampuni. Endapo kutakuwa na muda wa kutosha kabla ya tukio kuanza, Kampuni itajitahidi kuwasiliana na mteja na tunaweza, kwa hiari yetu wenyewe, kuruhusu chaguo la kufuta ubashiri.

10.3. Makosa katika Hesabu/Mstari/ Spreads/Handicap/ Jumla – Kabla ya kuanza tukio, wakati wa mchezo/ kucheza au baada ya tukio, endapo Kosa la Wazi litagundulika, ubashiri wote wa wazi utakubalika na utalipwa kwa hesabu, mstari, spreads, handicap au jumla iliyochukuliwa kwa kiasi kilichowekwa upya na Kampuni isipokuwa kwa matukio yafuatayo:

  • 10.3.1. Endapo kiasi kilichowekwa upya kinaonekana kuwa kidogo kuliko 1/10000 hivyo bashiri zitakuwa batili.
  • 10.3.2. bashiri yoyote inayowekwa kwenye hesabu, mstari, spread, handicap au jumla ambapo matokeo yameshajulikana wakati bashiri inawekwa, itakuwa batili.

10.4. Endapo kuna muda wa kutosha kabla ya tukio kuanza, Kampuni itajitahidi kuwasiliana na mteja na tunaweza kwa hiari yetu wenyewe, kuruhusu uchaguzi wa kufuta ubashiri.

10.5. Ratiba isiyo Sahihi – Endapo mchezaji au timu isiyo sahihi imetajwa sehemu ya majina ya ratiba, bashiri zote zitakuwa batili. Uamuzi huo utakuwa kwa hiari pekee ya Kampuni.

10.6. Mshiriki asiye Sahihi – Kama mshirika asiye sahihi ametajwa kwenye mechi yoyote au tukio, ubashiri utakaofanywa kwa mshiriki huyo utakuwa batili; washiriki wengine pia wanaweza kuwa batili. Uamuzi huo utakuwa kwa hiari ya Kampuni pekee.

10.7. Bashiri Zilizochelewa – Kama kwa sababu yoyote bashiri ya kabla ya tukio imekubaliwa kwa bahati mbaya baada ya mechi au tukio kuanza, bashiri zitalipwa kama ifuatavyo:

  • 10.7.1. Kama tukio na soko linakubalika wakati wa mchezo, basi bashiri zitakubalika kwa kiasi kipya kilichowekwa kwa muda ambao bashiri iliwekwa (ikiwa kiasi kipya kilichowekwa kinaonekana kuwa kidogo kuliko 1/20000 basi bashiri zitakuwa batili), isipokuwa kama matokeo yalishajulikana basi kwenye tukio hilo bashiri hizo zitakuwa batili.
  • 10.7.2. Kama tukio au soko halikubaliki wakati wa mchezo basi ubashiri utakubalika ilimradi mshiriki au timu iliyochaguliwa haijapata faida yoyote kubwa (mf. kupata goli, kutolewa kwa kadi nyekundu, nk.). Iwapo faida kubwa imepatikana, Kampuni itakuwa na haki ya kubatilisha ubashiri, ushindi au kukosa. Ubashiri wowote uliofanywa wakati matokeo yanajulikana, ikiwa ni pamoja na wakati wa mchezo, utakuwa batili.

11. HAKI MILIKI ZETU
+

11.1. Maudhui ya huduma ya Simu, Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS), Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki vinavyomilikiwa na Kampuni yanalindwa na Sheria za Kimataifa za Haki Miliki na haki miliki zingine. Mmiliki wa haki hizi ni Kampuni, Washiriki wake au Mtumwingine wa tatu ambaye ametoa leseni kwa Kampuni.

11.2. Bidhaa zote na majina ya Kampuni na nembo zilizotajwa katika Huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki ni alama za biashara, alama za huduma au majina ya biashara ya wamiliki wake husika, pamoja na Kampuni.

11.3. Isipokuwa kwa kiwango kinachohitajika kutumia bidhaa kwa madhumuni ya kufanya ubashiri au kuweka dau, hakuna sehemu ya Tovuti inayoruhusiwa kutolewa tena au kuhifadhiwa, kurekebishwa, kunakiliwa, kuchapishwa upya, kupakiwa, kuwekwa, kupelekwa au kusambazwa, kwa njia yoyote au kwa namna yoyote, au kuwekwa katika tovuti nyingine yoyote au kwenye mfumo mwingine wowote wa kurejesha wa kielektroniki wa umma au binafsi au huduma pamoja na ujumbe, miundo, video, ujumbe, namba na/au programu bila idhini yetu ya awali kwa maandishi.

11.4. Ukitumia kipengele kinachokuruhusu kupakia kitu, taarifa, maoni, matangazo au maudhui mengine katika huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki ('Maudhui ya Mtumiaji'), basi maudhui ya mtumiaji yatachukuliwa kuwa si ya siri na yasiyomilikiwa, na Kampuni ina haki ya kutumia, nakili, kusambaza na kutoa kwa mtu wa tatu Maudhui yoyote ya Mtumiaji kwa madhumuni yoyote. Kampuni pia ina haki ya kutoa utambulisho wako kwa mtu mwingine anayedai kuwa Maudhui yoyote ya Mtumiaji yaliyowekwa au kupakiwa nawewe katika huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, yana ukiukwaji wa haki miliki zao au wa haki yao ya faragha. Kampuni ina haki ya kuondoa, kurekebisha au kuhariri Maudhui yoyote ya Mtumiaji unayoweka kwenye huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki.

11.5. Matumizi yoyote ya kibiashara au utumiaji kupita kiasi wa Tovuti au maudhui yake ni marufuku kabisa. Kanuni hizi, Sera ya Faragha, kanuni na waraka wowote uliotajwa bayana na yoyote kati ya nyaraka hizo, na miongozo yoyote au kanuni zilizowekwa kwenye Tovuti vitakuwa ndio mkataba mzima na makubaliano ya wahusika na vinachukua nafasi ya mikataba yoyote ya awali kati ya Kampuni na wewe kuhusiana na mada hii. Unakiri na kukubali kuwa kwa kuingia katika na kukubali Kanuni hizi, Sera za Faragha, kanuni na waraka mwingine wowote uliotajwa wazi na yoyote kati ya nyaraka hizo, na miongozo yoyote au kanuni zilizowekwa katika huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, hauvitegemei, na havitakuwa na msaada kuhusiana na kauli yoyote, ahadi, dhamana, uelewa, ahadi au uhakika (ama kwa uzembe au bila kujua) na mtu yoyote (ama sehem ya mkataba huu au la) zaidi ya ilivyowekwa bayana katika nyaraka tajwa hapo juu. Kifungu hiki hakitatumika kumuondolea mtu kuwajibika kwa udanganyifu ama kauli zisizo za kweli.

12. KUZUIA UTAKATISHAJI FEDHA
+

12.1. Kampuni haitatumika na washiriki kutekeleza shughuli yoyote ya haramu, na wachezaji wote watafuata nidhamu ya hali ya juu na uadilifu katika uhusiano wao na Kampuni na watakuwa na wajibu wa kusaidia Kampuni kutekeleza vifungu vya Sheria ya Kuzuia Utakatishaji Fedha (Sheria Na. 12 ya Mwaka 2006) inayotumika Tanzania Bara na kama itakavyorekebishwa mara kwa mara pamoja na sheria na maazimio mengine husika.

12.2. Kampuni itafanya uchunguzi wa kina katika miamala yote ili kuzuia utakatishaji wa fedha pamoja na vitendo vingine haramu.

12.3. Endapo utapata taarifa juu ya vitendo vyovyote vinavyotia shaka kuhusiana na mtu (watu) binafsi, washiriki, wachezaji, maafisa au ya usahihi wowote au kutokufanya kazi vizuri kwa michezo, programu yake au vifaa, ni lazima uripoti vitendo hivyo au kutofanyika kwa vitendo hivyo kwa Kampuni mara moja.

12.4. Miamala yote inayotia shaka itaripotiwa kwenye Mamlaka husika na iwapo Kampuni itapata hasara yoyote ya kifedha ama madhara kwa jina lake au hadhi yake, njia zote za kisheria zitachukuliwa ili kutibu madhara kwa gharama ya mhusika.

12.5. Kampuni inaweza kusitisha, kuzuia au kufunga akaunti yako na kuizuia fedha kama inavyotakiwa na Sheria ya Kuzuia Utakatishaji Fedha (Sheria Na. 12 ya mwaka 2006) au sheria yoyote husika au kadri inavyoamriwa na mamlaka husika.

13. MALALAMIKO
+

13.1.Kama una malalamiko; tafadhali yatume kwenye kitengo chetu cha huduma kwa wateja kupitia barua pepe care@sportpesa.co.tz au piga +255764115588 au +255677115588 au +255685115588.

13.2. Kampuni itajitahidi wakati wote kufanya liwezekanalo kutatua tatizo lililoripotiwa mara moja.

13.3. Ikiwa una swali kuhusiana na muamala wowote, unaweza pia kuwasiliana na Kampuni kupitia care@sportpesa.co.tz au piga +255764115588 au +255677115588 au +255685115588 na kufafanua swali lako. Kampuni itapitia upya miamala yote yenye hoja au mgogoro.

13.4. Endapo kwa sababu moja ama nyingine haujaridhika na uamuzi wa Kampuni katika kutatua malalamiko yako, unaweza kupeleka malalamiko kwenye Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

13.5. Tafadhali elewa kuwa kwa kuwasilisha malalamiko yako kwenye Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, unathibitisha kwamba hujakiuka kanuni yoyote ya Kampuni kama ulivyokubali wakati wa kujisajili na Kampuni.

13.6. Kipindi kingine chochote ambapo mgogoro utajitokeza, wahusika watafikisha mgogoro huo kwaajili ya Uamuzi mbele ya Mwamuzi mmoja atakayekubalika na pande zote mbili ambapo eneo la utatuzi litakuwa Dar es Salaam. Ikiwa hakuna muafaka, kila upande utateua Mwamuzi na Waamuzi walioteuliwa watamteua Mwamuzi mmoja na iwapo hawawezi kukubaliana, mtu wa tatu atateuliwa na ambaye atamteua Mwamuzi huru.

14. KUCHEZA KWA WAJIBU
+

14.1 Kama Kampuni, tunaamini katika kutoa 'mazingira ya burudani salama'. Ni eneo muhimu sana katika mpango wetu wa jumla kuhakikisha huduma bora kwa wateja.

14.2. Michezo ya kubashiri katika mazingira salama inapaswa kuwa jambo la kusisimua na lenye furaha, kwa watu wazima. Tunataka ufurahie Kampuni, hivyo basi, tafadhali cheza kwa busara na ndani ya uwezo wako kifedha.

14.3. JIDHIBITI

  • 14.3.1: Idadi kubwa ya wateja wetu wanafurahia kupata burudani inayotolewa na Kampuni. Wakati wengi wao hucheza ndani ya uwezo wao, kwa wengine inaweza kuwa ni tatizo. Inaweza kukusaidia kujidhibiti kwa kuzingatia yafuatayo:
    • 14.3.1.1. Michezo ya kubashiri yapaswa kuwa jambo la kuburudisha na si kutengeneza fedha. Epuka kukimbizana na hasara;
    • 14.3.1.2. Chezea kiasi cha fedha unachoweza kumudu kukipoteza;
    • 14.3.1.3. Fuatilia muda na kiasi cha fedha unachotumia kwenye kamari;
    • 14.3.1.4 Ikiwa unataka kujipumzisha kucheza michezo ya kubashiri, unaweza kutumia huduma yetu ya kujitoa kwa kutuma barua pepe kwenda tz.customercare@sportpesa.com ukitoa taarifa za akuanti yako uliyofungua nasi. Kampuni itafunga akaunti yako/zako kwa muda wa miezi mitatu (3), kipindi ambacho hutoweza kufungua akaunti hiyo kwa sababu yoyote ile.

14.4. KUCHEZA KWA TATIZO

Endapo una wasiwasi kuwa kucheza michezo ya kubashiri kunaweza kuwa kumeteka maisha yako (au ya mtu mwingine) basi maswali yafuatayo yanaweza kukusaidia kutambua hilo:

  • 14.4.1. Je, watu wengine wameshawahi kukukosoa kuhusu uchezaji wako wa michezo ya kubashiri?
  • 14.4.2. Umeshawahi kusema uongo ili kuficha kiasi ulichochezea michezo ya kubashiri au muda uliotumia kucheza michezo ya kubashiri?
  • 14.4.3. Je, mabishano, kuchanganyikiwa au kukatishwa tamaa kunakufanya utake kucheza michezo ya kubashiri?
  • 14.4.4. Unacheza michezo ya kubashiri ukiwa peke yako kwa muda mrefu?
  • 14.4.5. Huendi kazini au chuo kwasababu ya kucheza michezo ya kubashiri?
  • 14.4.6. Unacheza michezo ya kubashiri kuepuka maisha yanayochosha au yasiyo na furaha?
  • 14.4.7. Unajishauri kutumia hela kwa kitu kingine isipokuwa kucheza michezo ya kubashiri?
  • 14.4.8. Umepoteza hamu kwa familia yako, marafiki au muda wa awali kutokana na michezo ya kubashiri?
  • 14.4.9. Baada ya kupoteza, unajisikia ujaribu haraka iwezekanavyo ili ushinde kiasi ulichopoteza?
  • 14.4.10. Unapocheza michezo ya kubashiri na kuishiwa pesa, je huwa unajihisi umekosa muelekeo na kujihisi mnyonge, na kuwa na haja ya kubashiri haraka iwezekanavyo?
  • 14.4.11. Je, unacheza michezo ya kubashiri hadi hela yako ya mwisho inakwisha?
  • 14.4.12. Umewahi kusema uongo, kuiba au kukopa ili upate pesa ya kucheza michezo ya kubashiri au pesa ya kulipa deni la michezo ya kubashiri?
  • 14.4.13. Unajihisi kuwa na mfadhaiko au hata kutamani kujiua kwasababu ya kucheza michezo ya kubashiri?

14.5. Maswali haya yametolewa ili kusaidia mtu kuamua kama ana tatizo na anahitaji kutafuta msaada.

14.6. Kupata Msaada: Kuna mashirika mengi ambayo yanaweza kutoa msaada kwa watu wanaopatwa na tatizo la kucheza michezo ya kubashiri. Kama unahisi imekutokea, tunakushauri kuwasiliana na shirika la kutoa msaada binafsi kwa muongozo zaidi.

15. MENGINEYO
+

15.1 Kampuni inafuatilia kikamilifu kuingia na kutoka katika Huduma za Simu, Tovuti na Vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki. Kampuni ina haki, kwa hiari yake yenyewe, kuzuia huduma endapo kutakuwa na ushahidi unaoonyesha kuwa kuna shughuli zinazojiendesha zenyewe au za ki-roboti.

15.2 Kampuni ina haki ya kuzuia upatikanaji wa baadhi au sehemu zote za huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki katika nchi kadha wa kadha.

15.3 Kampuni inaweza kubadilisha au kurekebisha bidhaa zinazotolewa kwa njia ya huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki wakati wowote na kwa sababu yoyote.

15.4 Mara kadhaa, sehemu chache au zote za huduma ya Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki zinaweza zisipatikane kwa ajili ya kutoa huduma husika. Endapo itatokea hivyo (kutopatikana) Kampuni haitowajibika kwa hasara au madhara yoyote ambayo mteja atapata.

15.5 Hakuna mazingira ambapo kuchelewa, kushindwa au kutofanya (kabisa au kwa kiwango fulani) katika kutekeleza, kufanya au kupigania haki yoyote, nguvu, upendeleo, madai au fidia iliyotolewa na au inayotokana na Kanuni hizi au sheria, itakuchuliwa kuwa au kutafsiriwa kama ni kusamehe kwa haki hiyo au haki nyingine yoyote, nguvu, upendeleo, madai au fidia kuhusiana na mazingira husika, au itumike kuzuia utekelezaji wa haki hiyo au haki nyingine yoyote, nguvu, upendeleo, madai au fidia, kwa namna nyingine yoyote wakati wowote au nyakati zijazo.

15.6 Haki na fidia inayotolewa na Kanuni hizi ni ya jumla tu na (isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo na Kanuni hizi) haiondoi haki au fidia nyingine yoyote iliyotolewa kwa mujibu wa sheria.

15.7 Endapo kipengele chochote cha Kanuni hizi kitakutwa na mahakama au chombo chochote chenye mamlaka kuwa batili au kisichotekelezeka, ubatili huo au kutokutekelezeka huko hakutoathiri vipengele vingine vya Kanuni, ambavyo vitabakia kutumika na kuwa na nguvu ileile.

15.8 Utathibitisha/kukubali na, pale ambapo ni lazima, utasaini au kuwezesha kusainiwa nyaraka zote na kufanya au kuwezesha kufanyika vitendo vingine vyote na vitu kurandana na Kanuni hizi ambavyo Kampuni inawaza, mara kwa mara, kuhitaji ili kuweka na kulinda faida zote za haki za Kampuni na faida zitakazohamishiwa au kutolewa kwa Kampuni chini ya Kanuni hizi na kwaajili ya kuzilinda na kuzitekeleza na vinginevyo kuvipa nguvu kamili vipengele vya Kanuni hizi.

15.9 Hakuna chochote katika Kanuni hizi kitatengeneza au kuonekana kutengeneza ushirika, ubia au mahusiano ya ki-wakala kati ya wahusika, na hakuna upande utakaokuwa na mamlaka ya kumfunga mwingine kisheria kwa namna yoyote isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo na Kanuni hizi.

15.10 Kampuni haitokuwa imekiuka Kanuni hizi wala kuwajibika kwa kuchelewa kutekeleza, au kushindwa kutekeleza, wajibu wake wowote, ikiwa kuchelewa huko au kushindwa kunatokana na matukio, mazingira au sababu zilizo nje ya uwezo wake ikiwemo (bila ukomo) kushindwa kokote kufanya kazi kwa mitandao ya mawasiliano ya simu, kukosekana kwa umeme, kushindwa kwa programu au vifaa vya kompyuta kwa mtu wa tatu, moto, radi, mlipuko, mafuriko, hali mbaya ya hewa, migogoro ya wafanyakazi au migomo, shughuli za kigaidi na vitendo vya Serikali au ya mmlaka nyingine husika. Katika hali kama hiyo, muda wa utekelezaji utaongezwa kwa kipindi sawa na kipindi ambacho utekelezaji wa jukumu ulicheleweshwa au ulishindikana kutekelezeka.

15.11 Kampuni inaweza kutoa, kuhamisha, kudai, kutoa leseni ndogo au kutumia Kanuni hizi kwa namna yoyote ile, au kutoa kwa njia ya mkataba haki au wajibu wowote chini ya Kanuni hizi kwa mtu yeyote ikiwemo kampuni yoyote ndani ya kundi la makampuni.

15.12 Notisi yoyote inayotakiwa kutolewa chini ya Kanuni hizi lazima iwe kwa maandishi, kwa lugha ya Kiingereza, na inaweza kufikishwa kwa mkono, au kwa njia ya posta ya daraja la kwanza, kupelekwa kwa njia ya posta kwa kusajili au kwa barua za ndege au nukushi kwenda:

  • 15.12.1. kwa upande wa Kampuni, anuani ya Kampuni kama iliyowekwa mwanzo kwa Kanuni hizi na mahala popote pengine; na
  • 15.12.2. kwa notisi zinazotolewa na Kampuni kwako, kwa mujibu wa utaratibu wa usajili wa mteja (pamoja na marekebisho ya maelezo uliyoyatoa kwa Kampuni);
  • 15.12.3. Notisi yoyote itachukuliwa kuwa imepokelewa:
    • 15.12.3.1. kama imefikishwa kwa barua pepe, ujumbe mfupi wa maneno, kwa mkono, wakati wa kufikisha.
    • 15.12.3.2 kama imetumwa kwa posta daraja la kwanza, kuandikisha wakati wa kupokea au kwa njia ya post kwa usajili, saa 8 mchana (Muda wa Tanzania) siku ya pili baada ya tarehe ya kutuma;
    • 15.12.3.3. kama imetumwa kwa njia ya ndege, siku ya tano baada ya tarehe ya kutuma; na(d) kama imetumwa kwa nukushi, wakati wa kupelekwa na mtumaji.

15.13. Viambatisho, Sera ya Faragha, kanuni na waraka wowote uliotajwa wazi na nyaraka hizi pamoja na miongozo au kanuni zilizowekwa kwenye tovuti, zitakuwa sehemu muhimu ya Kanuni hizi na zitakuwa na nguvu kana kwamba zimewekwa ndani ya Kanuni hizi.

15.14. Ikiwa kutakuwa na mgongano kati ya maudhui ya Kanuni hizi na Viambatanisho, Sera ya Faragha, kanuni na/au waraka wowote uliotajwa wazi na nyaraka hizi na miongozo au kanuni zilizowekwa kwenye huduma za Simu, Tovuti na vyombo vingine vya habari/majukwaa ya kielektroniki, Kanuni hizi zitatawala.

15.15. Endapo mchezaji atashinda, na kabla hajachukua zawadi yake akatangazwa kufariki, wategemezi wake au familia yake yawezapata zawadi hizo ikiwa tu watakuwa na amri halali ya mahakama, yaani barua za usimamizi wa mirathi ama idhinisho la kusimamia mirathi.

Mkeka

Namba za Malipo

  • 150888
  • 150888
  • 150888
  • 150888

Huduma kwa Wateja

Tunatoa huduma angalifu kwa wateja masaa 24 kwa wachezaji wa SportPesa.