Sera ya Faragha ya kampuni ya Sportpesa na Sera ya Kidakuzi
1. Kampuni ya Sportpesa yaweza wakati mwingine kuwa kama mdhibiti Taarifa na inaelewa kuwa faragha yako ni muhimu kwako na kwamba unajali namna taarifa zako zinavyotumika na zinavyohama kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine mtandaoni. Tunaheshimu na tunathamini faragha ya kila mtu anayetembelea Tovuti yetu na tutakusanya na kutumia taarifa kwa njia ambazo zina manufaa kwako na kwa namna inayoendana na haki zako na wajibu wetu chini ya sheria.
2. Sera hii inatumika kwa matumizi yetu ya data yoyote na data zote zilizokusanywa na sisi kuhusiana na matumizi yako ya Tovuti yetu. Tafadhali soma Sera ya Faragha hii kwa makini na uhakikishe kuwa unaielewa. Kukubaliana kwako na Sera yetu ya Faragha kunachukuliwa kutokea pale utumiapo tovuti yetu kwa mara ya kwanza NA/AU Utahitajika kusoma na kukubali Sera ya Faragha hii wakati unajisajili. Ikiwa hukubaliani na Sera ya Faragha hii, lazima uache kutumia Tovuti yetu mara moja.
3. Katika Sera hii maneno yafuatayo yatakuwa na maana zifuatazo:
"Akaunti" inamaanisha akaunti inayohitajika ili kufikia na/au kutumia maeneo fulani na vipengele vya Tovuti yetu;
"Kidakuzi" inamaanisha faili dogo la maandishi linalowekwa na Tovuti yetu kwenye kompyuta au kifaa chako pale unapotembelea sehemu fulani za Tovuti yetu na/au pale unapotumia sehemu fulani za Tovuti yetu. Maelezo zaidi ya Vidakuzi vinavyotumiwa na Tovuti yetu yamebainishwa katika kifungu cha 15, chini;]
"Tovuti yetu" inamaanisha tovuti hii, www.sportpesa.co.tz;
"Sheria ya Kidakuzi ya UK na EU" inamaanisha sehemu husika za Kanuni za Faragha na Mawasiliano ya Kielektroniki (Mwongozo wa EC) 2003, zilizorekebishwa mwaka 2004, 2011, 2015 na 2016 kama zilivyo katika tarehe ya Sera hii ya Faragha.
"Sheria ya Tanzania" inamaanisha Katiba ya Tanzania, Sheria ya Makosa ya Kimtandao, Sheria ya Miamala ya Ki-elektroniki na Sheria ya Mawasiliano ya Ki-elektroniki na Posta;
4. Tovuti yetu, www.sportpesa.co.tz inamilikiwa na kuendeshwa na Kampuni ya Sportpesa, Peninsula House, 251 Barabara ya Toure, Oystertabay, Kinondoni, Dar es Salaam.
5. Tovuti yawezafikiwa tu na watu walioko Tanzania.
6. Wigo - Je, Sera hii Inahusu Nini?
6.1 Sera hii ya Faragha inatumika tu kwa matumizi yako ya Tovuti yetu. Haitumiki kwa tovuti zozote zinazounganishwa kutoka kwenye Tovuti Yetu (iwe tumetoa viunganishi hivyo au vimetolewa na watumiaji wengine). Hatuna udhibiti wa namna taarifa zako zinavyokusanywa, kuhifadhiwa au kutumiwa na tovuti zingine na tunakushauri usome sera za faragha za tovuti hizo kabla hujatoa taarifa zozote kwao.
7. Ni Taarifa Gani Tunakusanya?
7.1. Badhi ya taarifa zitakusanywa moja kwa moja na Tovuti yetu kwa maelezo zaidi, tafadhali angalia kifungu cha 15 juu ya matumizi yetu ya Vidakuzi na Sera yetu ya Vidakuzi, taarifa zingine zitakusanywa tu ikiwa utaamua kwa hiari yako kuzitoa na kuridhia ili tuweze kuzitumia kwa madhumuni yaliyowekwa katika kifungu cha 8, kwa mfano, pale unapojisajili kwaajili ya kufungua Akaunti. Taarifa zaweza pia kukusanywa kutoka vyanzo vingine mbali na wewe ili kutusaidia kukuchunguza na pia kufanya upekuzi mwingine kama sehem ya kutekeleza wajibu wetu wa udhibiti. Kutegemeana na utumiaji wako wa Tovuti yetu, tunaweza kukusanya baadhi au taarifa zote zifuatazo:
a) Jina;
b)Tarehe ya Kuzaliwa;
c) Jinsia;
d) Wadhifa;
e) Taaluma;
f) maelezo ya mawasiliano kama anwani za barua pepe na namba za simu;
g) maelezo ya takwimu-watu kama vile msimbo wa posta, vipaumbele na vitu mtu anavyopendelea;
h) taarifa za kifedha kama vile namba za kadi za benki;
i) anwani ya IP (hukusanywa moja kwa moja)
j) aina ya kivinjari-tovuti na toleo (hukusanywa moja kwa moja);
k) mfumo unaotumiwa (hukusanywa moja kwa moja);
l) orodha ya URLs kuanzia tovuti uliyotoka, shughuli yako kwenye Tovuti Yetu, na tovuti unayoingia baada ya hapo (hukusanywa moja kwa moja);
8. Tunatumiaje Taarifa zako?
8.1 Taarifa zako zote binafsi zinahifadhiwa salama kwa mujibu wa sheria ya Tanzania na Kanuni ya jumla ya Utunzaji wa Taarifa ya EU (Kanuni (EU) 2016/679 (GDPR) pale inapofaa. Kwa maelezo zaidi juu ya usalama tazama kifungu cha 9, hapa chini
8.2. Tunatumia taarifa zako kukupatia huduma bora kabisa ya mtandao na pia huduma za mchezo wa kubashiri. Hii ni pamoja na:
8.2.1. Kukupatia na kusimamia Akaunti yako;
8.2.2. Kukupatia na kusimamia fursa ya kufikia Tovuti Yetu;
8.2.3. Kukupatia fursa ya kipekee na kuimarisha uzoefu wako kwenye Tovuti Yetu;
8.2.4. Utoaji bidhaa na huduma zetu kwako;
8.2.5. Kukupatia fursa ya kipekee na kuimarisha bidhaa na huduma zetu kwa ajili yako;
8.2.6. Kujibu mawasiliano kutoka kwako;
8.2.7. Kukutumia jumbe za barua pepe, kwa mfano, majarida, vidokezo na kadhalika ambavyo umekubali kuvipokea kwa kutiki kwenye kisanduku husika wakati unajisajili (unaweza kujitoa wakati wowote kwa kuwasiliana na care@sportpesa.co.tz au kutuma ujumbe mfupi "acha" au "ondoa" kwenda namba 15888;
8.2.8. Utafiti wa soko;
8.2.9. Kuchambua matumizi yako ya Tovuti yetu [na kukusanya maoni] ili kutuwezesha Kuendeleza Tovuti Yetu na uzoefu wako wa mtumiaji;
8.2.10. Kuhakikisha uhalali wa kusambaza huduma zetu katika eneo uliko;
8.2.11. Kupunguza udanganyifu, utapeli na hatari ya utakatishaji fedha;
8.2.12. Kufuatilia na kung'amua hatari ya ulevi wa kamari;
8.2.13. Kushirikiana na watu wengine mbali ya wewe kusaidia kuthibitisha utambulisho wako, uaminifu wako, chanzo cha fedha na utajiri wako dhidi ya vyanzo huru vya habari wanazoweza kuwanazo.
8.3. Wakati mwingine, ukusanyaji wa taarifa unaweza kuwa sharti la kisheria au la kimkataba, na Tunaweza kuwa tumefikia kikomo katika bidhaa na huduma ambazo Tunaweza kukupa bila ridhaa yako ili tuweze kutumia taarifa hiyo.
8.4. Kwa ruhusa yako na/au pale ambapo sheria imeruhusu, tunaweza pia kutumia taarifa zako kwa madhumuni ya kutangaza bidhaa zetu ambayo inaweza kuhusisha kuwasiliana nawe kwa njia ya barua pepe NA/AU simu NA/AU ujumbe mfupi wa maandishi NA/AU kukutumia taarifa, habari, na punguzo kwenye bidhaa zetu NA /AU huduma. Hata hivyo, hatutakutumia matangazo ya bidhaa zetu au ujumbe hewa bila kuomba na tutachukua hatua zote za kuhakikisha kwamba tunatetea kikamilifu haki zako na kuzingatia majukumu yetu chini ya sheria ya Tanzania na, pale ambapo inafaa, Kanuni za GDPR na Faragha na Mawasiliano ya Ki-elektroniki (Mwongozo wa EC) za mwaka 2003 kama zilivyorekebishwa mwaka 2004, 2011 na 2015.
8.5. Tutahakikisha kwamba taarifa zako binafsi zinachakatwa kihalali, kwa haki, na kwa uwazi, bila kuathiri haki zako. Tutachakata tu taarifa zako binafsi ikiwa kuna walau moja kati ya yafuatayo:
8.5.1. umetoa idhini ya kuchakata taarifa zako binafsi kwa lengo moja maalum au zaidi;
8.5.2. kuchakata taarifa zako ni muhimu ili kutekeleza wajibu chini ya mkataba ambao wewe ne sehem yake au ili kuchukua hatua kwa ombi lako kabla ya kuingia mkataba;
8.5.3. kuchakata taarifa zako ni muhimu ili kutekeleza wajibu wa kisheria ambayo tunawajibika kuitii;
8.5.4. kuchakata taarifa zako ni lazima ili kulinda maslahi yako muhim au ya mtu mwingine;
8.5.5. uchakataji ni muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa jambo ambalo linafanywa kwa maslahi ya umma au katika kutimiza wajibu wa kimamlaka aliopewa mtekelezaji; na /au
8.5.6. uchakataji ni muhimu kwa madhumuni ya kulinda maslahi halali ya kwetu au ya mtu wa tatu, isipokuwa pale maslahi hayo yanabatilishwa na haki za msingi na uhuru wa taarifa ambazo zinalinda utunzaji wa taarifa binafsi na haswa kama taarifa hizo zinamhusu mtoto.
9. Namna gani na wapi tunahifadhi taarifa zako?
9.1. Tunatunza tu taarifa zako kwa kadri tunavyohitaji ili tuweze kuzitumia kama ilivyoelezwa katika kipengele cha 8, na/au kwa kadri tupatavyo ridhaa yako ya kuzitunza. Vyovyote iwavyo, tutafanya marejeo kila mwaka ili kubaini kama tunahitaji kuendelea kutunza taarifa zako. Taarifa zako zitafutwa ikiwa hatuzihitaji zaidi kwa mujibu wa Sera yetu ya Usalama wa Taarifa na Sera ya Uhifadhi wa taarifa/data.
9.2. Baadhi au taarifa zako zote zitahifadhiwa nchini Tanzania. Unachukuliwa kukubali hili kwa kuanza kutumia Tovuti yetu na kuwasilisha taarifa Kwetu. Ikiwa Tunahifadhi au kuhamisha data nje ya Tanzania, tutachukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha kuwa taarifa zako zinachukuliwa kwa kama ambavyo ingekuwa ndani ya EEA na chini ya GDPR. Hatua hizo zinaweza kujumuisha, lakini sio tu, matumizi ya makubaliano ya kisheria baina yetu na watu wengine mbali na wewe Tunahusika katika matumizi ya Mipango ya Mikataba ya Mfumo wa Kupitishwa na EU. Tumeweka yafuatayo ili kulinda taarifa zako:
9.2.1. Uthibitisho huru kwamba mtu wa 3 anaetoa uthibitisho anatii GDPR na sheria ya Tanzania,
9.2.2. Vipengele muhimu vimekubaliwa na kuidhinishwa na EU,
9.2.3. Vipengele vya mkataba vinavyozungumzia udhibiti maaluma vinaendana na sera zetu za ndani kama ilivyotamkwa katika kifungu 9.2,
9.2.4. Ujumbe wa usalama na ulinzi wa taarifa zako wenye kiwango mahsusi cha utekelezaji,
9.2.5. Haki ya Ukaguzi
9.2.6. Usalama wa habari ni muhimu sana kwetu, na kulinda taarifa zako, tumeweka taratibu zinazofaa za kifizikia, za kielektroniki na utaratibu wa usimamizi wa kulinda na kuweka salama taarifa zilizokusanywa kupitia Tovuti Yetu.
9.3. Hatua Tunazochukua ili kuhakikisha na kulinda data yako ni pamoja na:
9.3.1. Timu ya wataalam waliojitolea kulinda usalama wa taarifa zako pamoja na shughuli zetu.
9.3.2. Mapitio ya kila mwaka na ukaguzi wa nje
9.3.3. Kutekeleza ISO 27001 na Mfumo wa Usimamizi wa Usalama wa Habari (ISMS)
9.3.4. Mradi wa uborehsji endelevu wa vidhibiti usalama vyote.
9.4. Bila kujali hatua za kiusalama tunazochukua, ni muhimu kukumbuka kuwa uhamisho wa taarifa kupitia mtandao waweza usiwe salama asilimia mia na kwamba unashauriwa kuchukua tahadhari stahiki unapotuma taarifa zako kwetu kupitia mtandao.
10. Je, Tunawapa watu wengine taarifa zako?
10.1. Tunaweza kuwapa taarifa zako makampuni mengine katika Kundi letu. Hii inajumuisha kampuni yetu Mama pamoja na makampuni Tanzu.
10.2. Tunaweza kuingia mkataba na watu wengine kukupatia bidhaa na huduma kwa niaba yetu. Hizi zaweza jumuisha mchakato wa malipo, utoaji wa bidhaa, vifaa vya kutafuta habari, matangazo na utafutaji masoko. Wakati mwingine, watu tunaowatumia wanawezahitaji kupata baadhi au taarifa zako zote. Iwapo taarifa yako yoyote itahitajika kwa dhumuni hilo, tutachukua hatua zote stahiki kuhakikisha kuwa taarifa zako zitachukuliwa kwa usalama na kwa mujibu wa haki zako, Wajibu wetu, na wajibu wa watu tunaowatumia chini ya sheria .
10.3. Tunaweza kukusanya takwimu kuhusu matumizi ya Tovuti yetu ikiwemo taarifa juu ya idadi ya watu wanaotumia Tovuti yetu, mifumo ya matumizi, namba za watumiaji, mauzo na habari zingine. Takwimu zote hizo zitakuwa za siri na hazitahusisha maelezo yoyote yanayofanya mtu kutambulika. Tunaweza mara kwa mara kuwapatia taarifa hizo watu wengine kama wawekezaji watazamiwa, washirika wetu, wabia na watangazaji. Taarifa zitatolea na kutumiwa kwa mujibu tu wa sheria.
10.4. Katika mazingira fulani Tunaweza kulazimika kisheria kutoa taarifa fulani tulizonazo, ambazo zinawezahusisha taarifa zako binafsi, mfano pale tunapokuwa sehem ya mashitaka ya kisheria, tunapotekeleza matakwa ya sheria ya Bunge, amri ya mahakama, au mamlaka ya serikali. Hatuhitaji idhini yoyote kutoka kwako ili kutoa taarifa zako katika hali kama hiyo na tutatii kama inavyotakiwa na ombi lolote la kisheria linalotolewa kwetu.
11. Je, Nini Kitatokea Iwapo Milki ya Biashara Yetu Itabadilika?
11.1. Tunaweza, mara kwa mara, kupanua au kupunguza biashara yetu na hii inaweza kuhusisha uuzaji na/au uhamisho wa udhibiti wa yote au sehemu ya biashara yetu. Taarifa zinazotolewa na watumiaji, ikiwa zitahitajika katika sehem yoyote ya Biashara yetu iliyohamishwa, zitahamishwa pamoja na sehemu hiyo na mmiliki mpya au mtu anayedhibiti biashara ataruhusiwa, kwa mujibu wa Sera ya Faragha hii, kutumia taarifa hizo kwa madhumuni yaliyokusudiwa awali wakati zikikusanywa.
11.2. Ikiwa Taarifa zako zitatakiwa kuhamishwa kwa sababu hiyo, tutawasiliana na kukutaarifu mapema kuhusu mabadiliko hayo.
12. Je, Unawezaje Kudhibiti Taarifa zako?
12.1 Unapowasilisha taarifa kupitia Tovuti yetu, unaweza kupewa fursa ya kuzuia namna tunavyotumia taarifa zako. Lengo letu ni kukupatia vidhibiti imara juu ya namna tunavyoweza kutumia taarifa zako (ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuchagua kutopokea barua pepe kutoka kwetu ambayo unaweza kufanya kwa kujiondoa kutumia viunganishi vinavyotolewa katika barua pepe zetu wakati wa kujisajili NA/AU NA/AU kwa kusimamia Akaunti yako).
13. Haki yako ya Kutotoa Taarifa na Haki Yako ya Kuondoa Taarifa Baada ya Kuitoa
13.1. Waweza wakati mwingine kufikia sehem fulani za Tovuti yetu bila kutoa Taarifa yoyote ile. Hata hivyo, ili kutumia sehem na vipengele vyote vinavyopatikana kwenye Tovuti yetu wawezatakiwa kuwasilisha au kuruhusu ukusanyaji wa taarifa fulani.
13.1.1. Unaweza kuzuia matumizi ya Vidakuzi vya kivinjari chako cha wavuti. Kwa habari zaidi, tazama sehemu ya 15 na Kiunganishi cha Sera yetu ya Kidakuzi.
13.1.2. Unaweza kuondoa ruhusa yako ya sisi kutumia Taarifa zako binafsi kama inavyoelezwa katika sehemu ya 8 wakati wowote kwa kuwasiliana nasi kwa kutumia maelezo yaliyotajwa katika kifungu cha 15. Hata hivyo, unakubali kuwa jambo hili linaweza kupunguza uwezo wetu wa kutoa bidhaa bora na huduma kwako.
14. Je, Wawezaje Kuzifikia Taarifa zako?
14.1 Una haki ya kisheria ya kuomba nakala yoyote ya Taarifa zako binafsi zilizohifadhiwa na sisi (kama zipo). Tafadhali wasiliana Nasi kwa maelezo zaidi katika care@sportpesa.co.tz na ulizia namna ya kupata huduma
15. Vidakuzi Gani Tunatumia na ni Kwa Nini?
15.1. Tovuti yetu inaweza kuweka na kufikia baadhi ya Vidakuzi vya awali kwenye kompyuta yako au kifaa. Vidakuzi vya awali ni vile vilivyowekwa moja kwa moja na sisi na hutumiwa tu na sisi. Tunatumia Vidakuzi ili kuwezesha na kuboresha uzoefu wako wa Tovuti yetu na kutoa na kuboresha bidhaa na huduma zetu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali angalia kifungu cha 8, hapo juu, na kifungu cha 15.5 hapa chini. Tumechagua hivi Vidakuzi kwa makini na tumechukua hatua za kuhakikisha kwamba faragha yako inalindwa na kuheshimiwa wakati wote.
15.2. Vidakuzi vyote vilivyotumiwa na kutumika kwenye Tovuti Yetu vinatumiwa kwa mujibu wa Sheria ya sasa ya Tanzania na Sheria ya Vidakuzi ya Uingereza na EU.
15.3. Kabla Vidakuzi vyovyote havijawekwa kwenye kompyuta yako au kifaa, kwa mujibu wa kifungu cha 15.5 NA/AU kifungu cha 15.7, utaonyeshwa ibukizi, mkanda wa ujumbe, na kadhalika, ukiombwa ridhaa yako ili kuweka Vidakuzi hivyo. Kwa kutoa ridhaa yako ili kuweka Vidakuzi, unatuwezesha kutoa uzoefu bora kabisa na huduma kwako. Unaweza, kama unataka, kukataa kutoa ridhaa ya kuweka Vidakuzi; hata hivyo baadhi ya sehem za Tovuti Yetu zinaweza zisifanye kazi sawasawa au kama ilivyokusudiwa. Utapewa fursa ya kuruhusu Vidakuzi vya awali tu na kuzuia Vidakuzi vingine.
15.4. Vipengele vingine vya Tovuti Yetu vinategemea Vidakuzi kufanya kazi. Sheria ya Kidakuzi ya Uingereza na EU imechukulia Vidakuzi hivi kuwa "vya lazima". Vidakuzi hivi vimeoneshwa hapa chini katika kifungu cha 15.5. Hatutohitaji Ridhaa yako ili kuweka Vidakuzi hivi. Bado unaweza kuzuia Vidakuzi hivi kwa kubadilisha mipangilio yako ya kivinjari cha mtandao kama ilivyobainishwa hapo chini katika kifungu cha 15.9, lakini tafadhali elewa kuwa Tovuti yetu inaweza isifanye kazi kama ilivyokusudiwa ikiwa utafanya hivyo. Tumechukua tahadhari kubwa ili kuhakikisha kuwa faragha yako haihatarishwi kwa kuruhusu Vidakuzi hivyo.
15.5. Vidakuzi vifuatavyo vya awali vinaweza kuwekwa kwenye kompyuta yako au kifaa chako:
Jina la Kidakuzi Lengo Muhimu Sana
spglobalssid Inatumika kufuatilia muda unaotumia kwenye Tovuti, kuzuia udanganyifu na kufanya uvinjari wako kuwa salama. Ndio
locale Inahifadhi lugha inayotumiwa/pendwa na mteja. Ndio
device_view Inahifadhi muonekano unaopendelewa na mteja. Ndio
cookies_consented Inatumika kurekodi na kukumbuka chaguo la mteja kwenye vidakuzi. Ndio
na vidakuzi vingine vifuatavyo vinaweza kuwekwa kwenye kompyuta yako au kifaa chako:
Jina la Kidakuzi Mtoa Huduma Lengo
_ga Google Taarifa za utambuzi wa Chambuzi za Google.
15.6 Tovuti yetu inatumia huduma za chambuzi zitolewazo na vichambuzi vya Google.Chambuzi za Tovuti maana yake ni mkusanyiko wa vifaa vinavyotumika kukusanya na kuchambua takwimu za matumizi, Kutuwezesha kuelewa zaidi namna watu wanavotumia Tovuti yetu. Hii, matokeo yake, inatuwezesha Kuboresha Tovuti yetu na bidhaa na huduma zetuzitolewazo kupitia Tovuti. Huhitaji kuturuhusu kutumia Vidakuzi hivi, kama inavyoonekana hapa chini, hata hivyo wakati Sisi kuvitumia haileti tishio lolote kwa faragha au utumiaji wa Tovuti yetu kwa salama, inatuwezesha kuendelea kuboresha Tovuti yetu na kuifanya bora zaidi na kuwa na kumbukumbu yenye manufaa kwako.
15.7 Huduma za Chambuzi (z)inazotumiwa na Tovuti yetu hutumia Vidakuzi kukusanya taarifa inayotakikana. Baadhi ya Vidakuzi hivi vinaweza kuwekwa mara tu unapotembelea Tovuti yetu kwa mara ya kwanza na yaweza kuwa vigumu sisi kupata ridhaa yako kabla. Waweza kuviondoa Vidakuzi hivi na ukazuia matumizi yake ya baadae kwa kufuata hatua zilizoainishwa hapa chini katika kifungu cha 15.9
15.8 Huduma za Chambuzi zinazotumiwa na Tovuti yetu hutumia Vidakuzi vifuatavyo:
Jina la Kidakuzi Chetu / Cha Wengine Mtoaji Lengo
_ga Wengine Google Taarifa za utambuzi wa Chambuzi za Google
15.9. Unaweza kuamua kuwezesha au kutowezesha Vidakuzi kwenye kivinjari chako cha wavuti. Vingi vya Vivinjari vya mtandao hukuwezesha pia kuamua ikiwa unataka kutowezesha Vidakuzi vyote au Vidakuzi Vingine pekee. Kwa namna vilivyotengenezwa, baadhi ya vivinjari vya mtandao hukubali Vidakuzi lakini hii inaweza kubadilishwa. Kwa maelezo zaidi, tafadhali angalia orodha ya usaidizi kwenye kivinjari chako cha mtandao au nyaraka zilizokuja na kifaa chako.
15.10. Unaweza kuchagua kufuta Vidakuzi wakati wowote hata hivyo unaweza kupoteza taarifa yoyote ambayo inakuwezesha kufikia Tovuti yetu kwa haraka na kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na, lakini sio tu, kuingia na mipangilio ya kibinafsi.
15.11. Inashauriwa kuwa na kivinjari cha wavuti na mfumo wa uendeshaji wa kisasa na pia kutembelea eneo la msaada na mwongozo viivyotolewa na msanifu wa kivinjari chako cha wavuti na mtengenezaji wa kompyuta au kifaa endapo huna uhakika kuhusu kurekebisha mipangilio yako ya faragha.
16. Haki zako kwa Kifupi chini ya sheria ya Tanzania na GDPR
Chini ya Sheria mbalimbali, una:
16.1. haki ya kuomba kupata, kufuta au kurekebisha, taarifa zako binafsi zilizohifadhiwa nasi;
16.2. haki ya kulalamika kwa mamlaka ya usimamizi;
16.3. kujulishwa kuhusu taarifa gani zinazochakatwa;
16.4. haki ya kuzuia mchakato wa taarifa;
16.5. haki ya usafirishaji taarifa;
16.6. kupinga uchakataji wa taarifa zako binafsi;
16.7. haki zihusianazo na mfumo huru wa maamuzi usioingiliwa pamoja na Taswira (tazama kifungu cha 17 hapa chini).
Haki hizo zinaweza zisitolewe zote ama zikawekewa utaratibu maalum wa kuzitekeleza kutokana na wajibu wetu wa udhibiti. Ili kutekeleza haki yoyote kati ya hizo hapo juu, au kama una maswali yoyote kuhusu Tovuti Yetu au Sera yetu ya Faragha, tafadhali wasiliana nasi kupitia maelezo yaliyotolewa katika kifungu cha 17 hapa chini. chini.
17. Mfumo huru wa Maamuzi na Taswira
17.1. Ikitokea tukatumia Taarifa zako binafsi kwa minaajili ya kufanya maamuzi huru ya moja kwa moja, na maamuzi hayo yana madhara ya kisheria (au madhara ya aina hiyo makubwa) kwako, una haki ya kupinga maamuzi hayo kwenye GDPR, ukiomba muingilio wa Binadamu, wakitoa mtazamo wao na kupata maelezo ya maamuzi kutoka kwetu.
17.2. Haki inayoelezwa katika kifungu cha 17.1 haitumiki katika mazingira yafuatazo:
17.2.1. Maamuzi ni muhimu ili kuingia katika, au kutekeleza mkataba baina Yako na Sisi;
17.2.2. Maamuzi hayo yameidhinishwa na sheria; au
17.2.3. Umetoa ridhaa yako wazi.
17.3 Pale tunapotumia Taarifa zako binafsi kwa minajili ya Taswira, yafuatayo yatazingatiwa:
17.3.1. Taarifa bayana inayoeleza kuwa Taswira itatolewa, ikieleza pia umuhimu wake na athari zinazoweza kujitokeza;
17.3.2. Taratibu madhubuti za kimahesabu au kitakwimu zitatumika;
17.3.3. Hatua za kiufundi na za kiofisi ambazo ni muhimu kupunguza uwezekano wa kutokea kwa makosa na kuwezesha makosa hayo kurekebishwa kirahisi zitachukuliwa; na
17.3.4. Taarifa zote binafsi zinazochakatwa kwaajili ya kujenga Taswira zitahifadhiwa ili kuepuka madhara ya kibaguzi yatokanayo na ujenzi wa Taswira.
17.4. Kwa sasa tunafanya maamuzi yanayojizalisha yenyewe yafuatayo:
17.4.1. PEPs na taarifa za wazi zinazoelezea juu ya ujenzi wa Taswira zitatolewa, ikiwemo umuhimu wake na athari zinazoweza kujitokeza;
17.4.2. Utakatishaji Fedha na Kufadhili mapambano dhidi ya Ugaidi;
17.4.3. Kufuatilia na kuibua ulevi wa Kamari
17.4.4. Utoaji wa viwango na odds.
17.5. Kwa sasa tunatengeneza Taswira ya taarifa zako binafsi kwa madhumuni yafuatayo:
17.5.1. Kuhakikisha uwepo wa toleo sahihi la kijiografia la jukwaa lako.
17.5.2. Kuhakikisha toleo sahihi kiufundi la jukwaa linapatikana
17.5.3. Kuhakikisha upatikanaji wa lugha sahihi ya jukwaa
17.5.4. Kuhakikisha odds sahihi zinatolewa
17.5.5. Kuhakikisha uwepo wa muda sahihi kwenye tovuti
17.6. Wasiliana Nasi
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu Tovuti yetu au Sera hii ya Faragha, tafadhali wasiliana nasi kwa njia ya barua pepe kwa care@sportpesa.co.tz, kwa simu (+255685115588 au +255692115588 au +255764115588), au kwa Sanduku La Posta 23135 Dar es Salaam. Tafadhali hakikisha swali lako linaeleweka, hasa ikiwa ni ombi la kupata maelezo kuhusu Taarifa tulizonazo kukuhusu wewe (kama ilivyo chini ya kifungu cha 14, hapo juu).
18. Mabadiliko kwenye Sera yetu ya Faragha
Tunaweza kubadilisha Sera hii ya faragha kwa kadri tunavyoona inafaa mara kwa mara, au kadri sheria inavyoweza kuhitaji. Mabadiliko yoyote yatawekwa mara moja kwenye Tovuti Yetu na utachukuliwa kukubaliana na masharti ya Sera ya Faragha pale utakapotumia Tovuti yetu kwa mara ya kwanza baada ya mabadiliko. Tunapendekeza uangalie ukurasa huu mara kwa mara ili kuwa na taarifa sahihi kila wakati.
Hakimiliki 2018 SportPesa
Imewezeshwa na tovuti mpya za Google, njia rahisi kuunda Tovuti nzuri.
Unda tovuti
Toa Taarifa kuhusu matumizi mabaya