Kucheza Michezo kwa wajibu

SportPesa imejitolea kuongeza ufahamu miongoni mwa wateja wake juu ya Kubashiri kwa kuwajibika. Mbali na hilo, inathibitisha ahadi yake ya, wakati wote, kutoa uzoefu mzuri wa kubashiri na wa kufurahisha kwa makundi yote yanayohusika wakati wowote. Wito huu wa kubashiri kwa kuwajibika haupo kwa lengo la kuwanyima wachezaji furaha wanayopata kutokana na kubashiri, lakini ni njia nzuri ya kuhakikisha kuwa mtu anakuwa na udhibiti.

https://sportpesa.co.tz/responsible_gaming 

Bashiri michezo yako kwa kuwajibika, na weka kiasi ambacho unaweza kumudu kukipoteza, kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa simu 0808 8020 133 au tembelea tovuti www.gamcare.org.uk.

Jidhibiti

Wateja wetu wengi wanafurahia kupata burudani ya Kampuni. Wakati wengi wao wanacheza michezo ya kubashiri ndani ya uwezo wao, kwa wengine michezo ya kubashiri inaweza kuwa ni tatizo. Inaweza kukusaidia kujidhibiti kwa kukumbuka yafuatayo:

a. Weka bashiri kiasi ambacho unaweza kumudu kukipoteza;

b. Zingatia muda unaotumia na pesa unazotumia kubashiri;

c. Kama unataka kuwa na mapumziko, unaweza kutumia uchaguzi wetu wa kujitengwa kwa kututumia barua pepe kwenda tz.customercare@sportpesa.com na maelezo ya akaunti uliyofungua nasi. muwakilishi wetu atakupigia kuthibitisha maelekezo yako na baada ya hapo Kampuni itafunga akaunti yako / zako kwa kipindi cha miezi 3, wakati ambapo itakuwa si rahisi kwa akaunti kufunguliwa kwa sababu yoyote ile.

Kubashiri kwenye michezo ni kuburudika na kusionekane kama njia ya kuingiza pesa; Epuka kupata hasara.

Endapo una wasiwasi kuwa kucheza michezo ya kubashiri kunaweza kuwa kumeteka maisha yako (au ya mtu mwingine) basi maswali yafuatayo yanaweza kukusaidia kutambua:

a. Je, watu wengine wameshawahi kukukosoa kuhusu uchezaji wako wa michezo ya kubashiri?

b. Umeshawahi kusema uongo ili kuficha kiasi ulichotumia kuweka ubashiri au muda uliotumia kucheza michezo ya kubashiri?

c. Je, malalamishi, kuchanganyikiwa au kukata tamaa kunakufanya utake kucheza michezo ya kubashiri?

d. Unacheza michezo ya kubashiri ukiwa peke yako kwa muda mrefu?

e. Hauendi kazini au chuo kwasababu ya kucheza michezo ya kubashiri?

f. Unacheza michezo ya kubashiri kuepika maisha yanayochosha au yasiyo na furaha?

g. Unajishauri kutumia hela kwa kitu kingine chochote isipokuwa kucheza michezo ya kubashiri?

h. Umepoteza hamu kwa familia yako, marafiki au muda wa awali kutokana na michezo ya kubashiri?

i. Baada ya kushindwa, unajisikia ujaribu haraka iwezekanavyo na kushinda ulichopoteza?

j. Ukiwa unabashiri na ukaishiwa pesa, je, huwa unajisikia kukosa mwelekeo na kukata tamaa, na kutaka kuweka ubashiri tena haraka iwezekanavyo?

k. Je, unaweka ubashiri ukitumia pesa zako zote?

l. Umewahi kusema uongo, kuiba au kukopa ili upate pesa ya kucheza michezo ya kubashiri au pesa ya kulipa deni la michezo ya kubashiri?

m. Unajihisi kuwa na mfadhaiko au hata kutamani kujiua kwasababu ya kucheza michezo ya kubashiri?

Maswali haya yametolewa ili kusaidia mtu kuamua kama ana tatizo na anahitaji kutafuta msaada.

Kupata Msaada

Kuna mashirika mengi ambayo yanaweza kutoa msaada kwa watu wanapatwa na tatizo la kucheza michezo ya kubashiri. Kama unahisi imekutokea, tunakushauri kuwasiliana na shirika la kutoa msaada binafsi kwa muongozo.

Kizuizi cha kubashiri kwa walio chini ya umri

Hairuhusiwi kwa walio chini ya umri wa miaka 18 kubashiri.

Namna ya kuwalinda walio chini ya umri dhidi ya kubashiri:

Taarifa zako kama vile amana, neno la siri na jina la mtumiaji visiwekwe wazi kwa walio chini ya umri.

Mashine yako isibaki bila usimamizi wakati umeingia. Epuka kutumia uchaguzi wa "Kumbuka Neno langu la Siri" kwenye kompyuta yako.

Funga kompyuta yako kwa neno la siri ili kudhibiti au kuzuia kuingia kwenye kompyuta kwa bahati mbaya.

Wafahamishe watoto wako juu ya hatari za kubashiri kwa watu walio chini ya umri.

Vinginevyo, tumia programu zenye kuwalinda watoto.

Tahadhari tulizoweka ili kuzuia kubashiri kwa walio chini ya umri:

Kila mtu anayejiunga ili kupata akaunti mpya katika www.sportpesa.co.tz atalazimika kuweka tiki kwenye kiboksi kinachosema kuwa ana umri wa miaka 18 au zaidi. Kuna taarifa kuwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 18 hawaruhusiwi.

Pale ambapo mtu ametengeneza akaunti kutumia tarehe yake y kuzaliwa, anuani na jina, taarifa hizo zitatumika kutambua kuwa mtu huyo ana umri zaidi ya miaka 18.

Kutumia Pasi yako ya kusafiria au Kitambulisho halali cha Taifa wakati wa kutoa pesa kutoka kwa mtoa huduma yoyote wa mtandao wako Tanzania, ni tahadhari nyingine ya uhakiki.

Huduma zetu za malipo zipo kulingana na huduma za fedha kwa njia ya simu. Kujisajili kupata huduma hizo, kisheria, mtu analazimika kuwa na umri wa miaka 18 au zaidi, na awe na Kitambulisho halali cha Taifa. Kwa malipo ya hundi au fedha taslimu, tutahitaji ushahidi wa umri kupitia kitambulisho.

Endapo utahisi au kujua mtoto yoyote ambaye anacheza michezo ya kubashiri kwenye majukwaa yetu au kutumia akaunti ya mu mwingine, tufahamishe mara moja kupitia tz.customercare@sportpesa.com kwa hatua muhimu kuchukuliwa. Maelezo yako yatakuwa ya siri na juhudi yako itashukuriwa.

Kufuata mipaka

Majukwaa yote ya SportPesa yana kikomo cha kiwango cha juu cha TZS 500,000 kwa bet moja.

Mapitio ya historia ya mteja mara kwa mara

Ili kuweza kufuatilia shughuli zako za kubet kwenye SportPesa, tunakupa urahisi wa kupata historia ya shughuli za miamala yako ya kila mwezi. Bonyeza kwenye “Historia ya Kubet” kwenye akaunti yako ya www.sportpesa.co.tz, kufuatilia bet ulizoweka, pesa ulizotoa na ulizoweka. Aidha, salio la akaunti yako ya SportPesa daima huonyeshwa kwenye kona ya juu upande wa kulia wa skrini yako, unapoingia kwenye akaunti yako.

Chaguzi la Kujitoa

Huduma ya kujitoa ya SportPesa inakuruhusu kufunga akaunti yako kwa muda fulani.

Wakati wa kujitoa, hautoruhusiwa kufungua tena akaunti yako au akaunti nyingine mpya.

Utaratibu wa ufuatiliaji utawekwa kwa shughuli yoyote inayohusiana na akaunti yako au wasifu wako kwenye majukwaa ya kubashiri ya SportPesa. Akaunti zozote mpya zitakazohisiwa zitafungwa mara moja.

Namna gani ya kuomba kujitoa kwenye Sportpesa?

Tuandikie barua pepe kwenda tz.customercare@sportpesa.com kuomba kufungiwa akaunti yako kwa muda fulani ambao ungependelea.

Mara baada ya kutuma ombi lako, wawakilishi wetu watawasiliana na wewe kuthibitisha ombi lako na utapokea barua pepe itakayothibitisha kuwa tumepata ombi lako. Hii huwa ndani ya saa 48 za kutuma ombi la Kujitenga.

Je, mchakato wa Kufunga Akaunti unahusisha nini?

Mara baada ya kupokea ombi la kujitenga, mchakato wa kufunga akaunti utaanza. Hasa unahusisha kuangalia salio la akaunti au bet zozote zinazosubiri na kufunga akaunti; pamoja na kuweka tahadhari juu ya shughuli yoyote itakayohusiana na akaunti husika au wasifu kwenye majukwaa ya kubashiri ya SportPesa.

Inachukua muda gani kuamilishwa mara baada ya kuomba kujitenga?

Utaratibu huu unahitaji kipindi fulani cha kufanya kazi ili kutekeleza. Hata hivyo, tutajitahidi kukamilisha kujitenga kwako haraka iwezekanavyo. Kwa kawaida, itachukua muda usiozidi saa 48 kutekeleza baada ya kupokea barua pepe inayothibitisha kupokea ombi la kujitenga juu ya akaunti yako kutoka kwa Wakala wa SportPesa. Mara baada ya mchakao wa kufunga Akaunti kukamilika, utapata barua pepe ya uthibitisho kukutahadharisha juu ya kufungwa muda mfupi. Kipindi cha kujitenga kinachukuliwa kuwa kimeanza pale utakapofahamishwa.

Ni nini kinachotokea kwenye salio langu lililopo katika akaunti yangu ya SportPesa baada ya kufungwa kwa muda?

Kama una fedha zozote, tutawasiliana na wewe ili uzitoe au utupe ridhaa kuwa unataka pesa zibaki katika akaunti yako.

Nini kitachotokea kwa bet nilizoweka ambazo bado hazijafikiwa hitimisho?

Bet zozote ambazo hazijashughulikiwa zitashughulikiwa kwenye matokeo ya tukio hilo. Kama bet yako imeshinda, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya Msaada kwa Wateja ili kupanga juu kufanya malipo ya ushindi wako.

Nifanyeje kama bado naweza kuingia kwenye akaunti yangu ya SportPesa baada ya kipindi cha kujitenga kuanza?

Kama bado unaweza kupata huduma zetu zozote za SportPesa baada ya kupokea mawasiliano ya kuamilishwa kwa kipindi cha kujitenga, tafadhali tufahamishe mara moja. Tuandikie kwenda tz.customercare@sportpesa.com utufahamishe kuhusiana na kuendelea kupata huduma za SportPesa.

Ukishindwa kutufahamisha, hatutawajibika kwako au kwa mhusika wa upande wa tatu kama unaweza kuendelea kubet kupitia tovuti ya SportPesa au kwa UJUMBE au kwenye majuwaa yetu mengine baada ya kujitenga.

Nifanye nini wakati wa kipindi cha kujitenga?

Tunashauri utafute msaada wa ziada na ushauri wakati wa kupindi cha kujitenga. Mara baada ya muda kuisha, tutafungua akaunti yako.

Mkeka

Namba za Malipo

  • 150888
  • 150888
  • 150888
  • 150888

Huduma kwa Wateja

Tunatoa huduma angalifu kwa wateja masaa 24 kwa wachezaji wa SportPesa.